MAMBO MATATU(3) YANAYOAMBATANA NA TOBA YAKO YA KWELI.
BWANA YESU atukuzwe ndugu yangu.
Karibu tujifunze Neno la MUNGU la uzima.
Leo nazungumzia TOBA.
BWANA YESU alikuja kwa ajili ya wanadamu watubu na kurudi katika miliki ya MUNGU kwa ajili ya uzima wa milele.
Luka 5:32 '' Sikuja kuwaita wenye haki, bali wenye dhambi, wapate kutubu. ''
-Kutubu ni kugeuka kutoka kwenye dhambi na kuingia kwenye utakatifu.
-Kutubu ni kuomba msamaha kwa MUNGU na baada ya kuomba msamaha unaacha
dhambi zote ikiwemo na ile iliyosababisha ukaomba msamaha.
-Kutubu ni mabadiliko katika mtazamo, kutoka mtazamo mbaya na kuingia katika mtazamo mzuri.
-Kutubu ni kutafuta kumpendeza MUNGU.
-Kutubu ni kujitenga na dhambi zote huku ukiambatana na KRISTO YESU.
-Kutubu ni muhimu sana.
Luka 15:7 '' Nawaambia, Vivyo hivyo kutakuwa na furaha mbinguni kwa
ajili ya mwenye dhambi mmoja atubuye, kuliko kwa ajili ya wenye haki
tisini na kenda ambao hawana haja ya kutubu. ''
Mimi Peter Nilipookoka jambo la kwanza nilianza kuharibu vitu vyangu ambayo havimpendezi MUNGU, Ufahamu wangu kumbe kabla ya kuokoka haukujua
mambo mambo mazuri. nilikusanya CD zangu zote na kukuta sina hata CD au
DVD moja ya nyimbo za injili wala mahubiri, DVD zangu zote zilikuwa ni
miziki tu ya kidunia na filamu tena filamu mbaya mbaya, nilizichukua na
kuanza kuvunja, rafiki yangu mmoja aliniona na kunishangaa na kuniambia
nimpe yeye lakini nilikataa na kuzivunja zote na kuna vitabu vya mambo
mabaya nilivichoma moto. Video zote za ngono na picha kwenye simu yangu
nilifuta maana nilidhamilia haswaaaaa kumpendeza MUNGU.
Toba ya kweli ndugu zangu huambatana na mabadiliko yatakayodumu siku zote za maisha yako.
2 Petro 3:9 '' BWANA hakawii kuitimiza ahadi yake, kama wengine
wanavyokudhani kukawia, bali huvumilia kwenu, maana hapendi mtu ye yote
apotee, bali wote wafikilie toba.'
'
MAMBO 3 YANAYOAMBATANA NA TOBA YA KWELI.
1. TOBA YA KWELI HUAMBATANA NA KUBADILIKA NIA..
Warumi 12:2 '' Wala msiifuatishe namna ya dunia hii; bali mgeuzwe kwa
kufanywa upya nia zenu, mpate kujua hakika mapenzi ya MUNGU yaliyo mema, ya kumpendeza, na ukamilifu. ''
-Baada ya kutubu dhambi lazima
ubadilishe nia yako kutoka nia ya dhambi na kuingia katika nia ya
utakatifu. kuna mtu kila siku hufanya uzinzi na kila siku hutubu, hiyo
sio toba ya kweli maana nia yake haijabadilika. Nia ikibadilika
hutaruhusu tena dhambi ambazo zilikutesa kabla hujatubu. kama nia yako
imekuwa nia safi hakika huwezi hata kukaa katika bar ambayo kila siku
ulikuwa unashinda pale kabla hujatubu kwa BWANA YESU. Kama nia yako
isipobadilika hakika kila siku utakuwa unajikwaa katika lilelile
unalolitubia na hapo unakuwa hujatubu toba ambayo inampendeza MUNGU.
Mathayo 15:19 ''Kwa maana moyoni hutoka mawazo mabaya, uuaji, uzinzi, uasherati; wivi, ushuhuda wa uongo, na matukano; ''
-Ukibadilika nia kutoka nia kuwaza uzinzi na uasherati hakika
utafanikiwa kuingia katika toba ya kweli. kama mabaya hayo bado yako
moyoni mwako hakika utajikuta tu unayatenda tena maana bado wewe ni
mtumwa wa dhambi hizo.
-Ukitubia dhambi fulani hakikisha unabadilika nia ya kufuata dhambi hiyotena.
Waebrania 8:10b '' Nitawapa sheria zangu katika nia zao, Na
katika mioyo yao nitaziandika; Nami nitakuwa MUNGU kwao, Nao watakuwa
watu wangu. ''
-Katika nia yako MUNGU huweka sheria yake yaani
huweka kila jambo ambalo unatakiwa uliendee au uliishi baada ya hapo.
Sheria hiyo MUNGU huitoa kupitia watumishi wake na neno lake Biblia
takatifu . baada ya kutubu unatakiwa usitende dhambi tena hiyo ndio
sheria ya MUNGU kwako.
2. TOBA YA KWELI HUAMBATANA NA KUBADILIKA MTAZAMO.
Yohana 15:4 '' Kaeni ndani yangu, nami ndani yenu. Kama vile tawi
lisivyoweza kuzaa peke yake, lisipokaa ndani ya mzabibu; kadhalika
nanyi, msipokaa ndani yangu.''.
-BWANA YESU hapo anaposema kwamba tukae ndani yake maana yake tusiondoke ndani yake kimtazamo na kimatendo.
-Huwezi kusema umetubu halafu mtazamo wako ukabaki kwamba hakuna haja
ya kwenda kanisani wala kujifunza Neno la MUNGU. Ndugu ukifanya hivyo
hutafika popote utajikwaa tu na kuirudia dhambi ambayo ilikufanya utubu.
toba ya kweli ni pamoja na kubadilika mtazamo kutoka mitazamo mibaya na kuingia katika mtazamo mzuri ambao ni kukaa ndani ya YESU.
Kukaa ndani ya YESU ni;
-Kukaa katika Fundisho lake.
-Kukaa katika Wokovu wake.
-Kukaa katika Neno la MUNGU na maombi.
-Kukaa katika mapenzi yake.
-Kukaa katika utakatifu.
-Kukaa katika upenndo wa wake.
-Kukaa katika Imani pasipo kuondoka wala kuhama.
1 Kor 15:33-34 '' Msidanganyike; Mazungumzo mabaya huharibu tabia
njema. Tumieni akili kama ipasavyo, wala msitende dhambi; kwa maana
wengine hawamjui Mungu. Ninanena hayo niwafedheheshe.''-Kama bado mtazamo wako uko katika kujumuika na marafiki zako watenda
dhambi katika eneo lile lile lililokuwa linasababisha kutenda dhambi
basi utajikuta tu unaanguka tena na tena katika dhambi.
-Kama mtazamo wako ni kwamba unatubu kisha unajitenga na kanisa hakika hutafika popote bali utaanguka tu dhambini.
Toba halisi ni pamoja na kubadilika mtazamo. kuna watu mtazamo wao ni
kwamba kwenda disko kujirusha na kucheza ni jambo jema wakati mtazamo
huo ni wa shetani maana ukiwa katika maeneo hayo utajikuta una ''onja
ila usilewe'' kumbe ni usanii tu wa shetani. disko utajikuta unatamani
watu wasiokuhusu maana upo katika uwepo wa shetani. Mtazamo kama huo
lazima ubadilike ndipo toba yako itakaa maana adui hatapeleka mashitaki
yeyote kuhusu wewe.
3. TOBA YA KWELI HUAMBATANA NA KUFANYA MABADILIKO KATIKA JINSI YA KUISHI.
2 Thesalonike 1:9-10 '' Kwa kuwa wao wenyewe wanatangaza habari zetu,
jinsi kulivyokuwa kuingia kwetu kwenu; na jinsi mlivyomgeukia MUNGU
mkaziacha sanamu, ili kumtumikia MUNGU aliye hai, wa kweli; na kumngojea
Mwanawe kutoka mbinguni, ambaye alimfufua katika wafu, naye ni YESU,
mwenye kutuokoa na ghadhabu itakayokuja. ''.Huu ni mfano wa yule aliyebadilika baada ya toba na kuacha na maisha ya
kuabudu sana au kusujudia. Kama alikuwa na sanamu nyumbani mwake ambayo
kila siku alikuwa anaibussu na kuisujudia baada ya toba ya kweli
anachoma moto sanamu hizo, hayo ndio matokeo halisi ya toba ya kweli.
-Kama ulikuwa mganga wa kienyenyi baada ya toba unabadilika na kuchoma
moto zana zote za uganga na kuanza kuishi maisha mapya matakatifu mbele
za MUNGU BABA, Hiyo ndio toba ya kweli.
-Kama ulikuwa unaroga watu
au kuwatapeli, baada ya kumpokea YESU na kutubu unaamua kuharibu zana
zote za uchawi ulizokuwa nazo, hayo ndio matokeo ya toba ya kweli.
-Haiwezekani mfano kijana mzinzi anaamua kumpokea YESU na kutubu kisha
kuacha uzinzi lakini nyumbani kwake ana pakti 3 za kondomu na kila siku
huvaa moja kwa kijifurahisha na pia ana kitabu cha picha za x na katika
laptop yake amejaza filamu za ngono. mtu wa hivyo kama anajishughulisha
na vitu hivyo vitamnajisi tu na kujikuta akirudi tena dhambi.
Mathayo 3:8 '' Basi zaeni matunda yapasayo toba;''
-Ndugu, ni matunda gani au ni mambo gani yanazaliwa baada ya wewe kutubu? je unazaliwa utakatifu wa kudumu au utakatifu wa muda tu?
Ndugu nakushauri zaa matunda/matendo mazuri baada ya kutubu.
KAMA UNATAKA KUTUBU RUDIA MANENO HAYA KISHA TAFUTA KANISA LA KIROHO UKAJIUNGE NA KUANZA KUISHI MAISHA MATAKITI.
''BABA katika jina la YESU KRISTO Niko mbele zako mimi mwenye dhambi,
lakini leo nimetambua kosa langu na naomba unisamehe dhambi zangu zote,
nisamehe dhambi ninazozikumbuka na pia zile ambazo sizikumbuki. futa
jina langu katika kitabu cha hukumu na uliandike jina langu katika
kitabu cha uzima. Neno lako katika Warumi sura ya 10 Mstari wa 9 na wa
10 Neno lako linasema ''Kwa sababu, ukimkiri YESU kwa kinywa chako ya
kuwa ni BWANA, na kuamini moyoni mwako ya kuwa MUNGU alimfufua katika
wafu, utaokoka. Kwa maana kwa moyo mtu huamini hata kupata haki, na kwa
kinywa hukiri hata kupata wokovu '' . BWANA YESU mimi nimekuamini leo na
hivyo naamini sasa napokea wokovu wako na hakika nimeokoka. Kuanzia leo
Naufunga ukurasa wa dhambi na ninaufungua ukurasa wa matendo mema na
matakatifu. BWANA nipe ROHO wako Mtakatifu ili aniwezeshe kushinda
dhambi na anasa zote za dunia. Kuanzia leo mimi nimeokoka na ni mtoto wa MUNGU mwenye haki zote. ninafuta laana
zote na kila roho ya shetani inayonifuatilia naiharibu kwa jina la YESU
KRISTO kama neno la MUNGU linavyosema katika Yeremia sura ya kwanza
mstari wa 10. BWANA YESU nakushukuru sana kwa kuniokoa. Yote haya kwa
imani nimepokea na niko tayari sasa kwa ROHO MTAKATIFU kunitumia. Katika
jina la YESU KRISTO nimeomba na kupokea Amen.
Kama umetubu toba ya kweli hakika wewe kuanzia sasa ni mshindi na ni shujaa.
Kwa sasa naishia hapo, MUNGU akitupa nafasi tutajifunza tena siku
nyingine. ulishindwa kumpokea BWANA YESU nafasi yako bado ipo na muda wa
kumpokea ni leo wala sio kesho, amua leo na atakuandika jina lako
katika kitabu cha uzima na utaanza kuukulia wokovu kwa mafundisho
kanisani. MUNGU ana makusudi kabisa na wewe, hataki upotelee motoni
anataka uende uzimani aliko KRISTO BWANA. MUNGU akubariki sana .
Saturday, 28 October 2017
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
KAZI KUU TANO (5) ZA IMANI KATIKA MAOMBI.
Bwana YESU atukuzwe ndugu zangu. Karibu tujifunze Neno la MUNGU. Uhusiano ni upendo unaozaa ushirikiano na mawasiliano kati ya pande m...
-
Bwana YESU atukuzwe ndugu zangu. Karibu tujifunze Neno la MUNGU. Uhusiano ni upendo unaozaa ushirikiano na mawasiliano kati ya pande m...
-
Bwana Yesu asifiwe… Imeandikwa ; “ Bali wote waliompokea aliwapa uwezo wa kufanyika watoto wa Mungu, ndio wale waliaminio jina lake; “Y...
-
Ni miaka mingi nimekuwa nikijiuliza swali hili, nitawezaje kumpenda Mungu kwa moyo wangu wote, kwa akili zangu zote na kwa nguvu zangu zote...
No comments:
Post a Comment