MUNGU ANATAKA KABLA YA YOTE KWANZA TOBA YA KWELI.
BWANA YESU asifiwe ndugu yangu.
Karibu tujifunze habari za uzima wa roho zetu.
Neno la MUNGU ni chakula za roho zetu hivyo kwa vyovyote vile kama
tunataka tuwe hai kiroho lazima tu tujifunze Neno la MUNGU aliye hai.
MUNGU yuko hai na Neno lake liko hai vilevile.
Kama kuna jambo gumu kwa watu wengi basi ni toba ya kweli yaani kutubu na kuacha dhambi hiyo.
Siku zote na miaka yote MUNGU anataka sana watu wake watubu na kugeuka
yaani watubu na kuacha dhambi hizo. Maana yake kama unafanya uzinzi na
kutubu kila siku na baadae unarudi tena kwenye uzinzi hapo bado
haikusaidii, tena hujatubu, huko ni kumjaribu MUNGU na Biblia iko wazi
kabisa kwamba ''Usimjaribu BWANA MUNGU wako-Luka 4:12) MUNGU hajaribiwi kwa uovu, unatenda dhambi ukijisemea ''si
nitatubu''.Ndugu hata wote walio matesoni kuzimu leo walijisemea hivyo
hivyo unavyojisemea wewe lakini walijikuta huko bila kutubu toba la
kweli.
Kama kuna mahubiri MUNGU anataka watumishi wake wahubiri
kila iitwapo leo basi nikuhubiri ili watu watubu na kumpokea YESU KRISTO
na majina yao yataandikwa kwenye kitabu cha uzima.
-Kutubu ni muhimu sana.
-Hakuna dhambi inayojisamehe yenyewe ndugu zangu.
-Hakuna kusamehewa kwa njia ya sms tu ya kuambiwa ''umesamehewa dhambi zako''
-Hakuna kusamehewa kwa njia ya kutoa pesa za kitubio, kitubio cha pesa ni ushetani.
-Hakuna kutubu baada ya kufa.
-Hakuna maombi ya mtu awaye yeyote yanayoweza kumbadilishia makazi marehemu yeyote.
MUNGU anataka wewe mwenyewe mwenye dhambi uchukue maamuzi, Wachungaji kazi yao ni kuwapatanisha wanadamu na MUNGU aliye hai
kupitia YESU KRISTO. Ni jukumu lako kuongozwa kwa maombi na jina lako
litaandikwa tena kwenye kitabu cha uzima mbinguni. Kuna mambo makuu matatu nataka niyazungumzie katika ujumbe wa leo.
=Jambo la kwanza ni kwamba Yohana mbatizaji alipoanza tu kuhubiri,
Jambo la kwanza alisema '' Tubuni; kwa maana ufalme wa mbinguni
umekaribia.- Mathayo 3:2 ''
-Unaweza ukajiuliza, Kama Yohana
mbatizaji angekuwa baadhi ya wahubiri wa leo angeanza huduma yake kwa
mahubiri yasemayo ''Njoni kwangu ili mbarikiwe kwa baraka kubwa kubwa za
nyumba na magari''
Lakini MUNGU anataka kwanza toba, Lengo la
BWANA YESU ni watu wampokee na kutubu ili wapate nafasi ya uzima wa
milele. ''YESU akamwambia, Mimi ndimi njia, na kweli, na uzima; mtu haji
kwa Baba, ila kwa njia ya mimi -Yohana 14:6''
Yohana alimtii ROHO MTAKATIFU ndio maana alihubiri toba.
=Jambo la pili ni kwamba BWANA YESU alipoanza huduma yake hapaDuniani alianza na jambo hilo hilo, Mathayo 4:17 Biblia inasema ''
Tokea wakati huo YESU alianza kuhubiri, na kusema, Tubuni; kwa maana
ufalme wa mbinguni umekaribia. '' -YESU anaanza kuwahubiri watu
kwa kuwaambia watubu maana ufalme wa MUNGU umekaribia. Na Katika Marko
Biblia inasema '' Hata baada ya Yohana kutiwa gerezani, YESU akaenda
Galilaya, akiihubiri Habari Njema ya MUNGU, akisema, Wakati umetimia, na
ufalme wa MUNGU umekaribia; tubuni, na kuiamini Injili.-Marko 1:14-15''
-BWANA YESU anaanza tu huduma kwa kusema ''Tubuni na kuiamini injili kwa maana Ufalme wa MUNGU umekaribia''
-Toba ni jambo kuu ambalo MUNGU analihitaji kwako na kwangu ndugu, sio
kwamba injili za mafaniko ni mbaya hapana ila muhimu kuliko yote ni Toba
na jambo la toba ndilo linalotakiwa lipewe nafasi ya kwanza kuliko
yote.
=Jambo la Tatu ambalo nataka nizungumzie ni Mitume
walipoanza tu kuhubiri injili, moja ya maneno ya kwanza kusemwa na wao
ni hili hapa '' Tubuni basi, mrejee, ili dhambi zenu zifutwe, zipate
kuja nyakati za kuburudishwa kwa kuwako kwake BWANA; apate kumtuma
KRISTO YESU mliyewekewa tangu zamani; ambaye ilimpasa kupokewa mbinguni hata zije
zamani za kufanywa upya vitu vyote, zilizonenwa na MUNGU kwa kinywa cha
manabii wake watakatifu tokea mwanzo wa ulimwengu-Matendo 3:19-21'' -Hata mitume walianza na mafundisho ya toba.
Toba ni muhimu sana maana baraka bila kutubu hakuwezi kumwepusha mtu na
jehanamu, lakini toba ya kweli ndiyo inayoweza kumwepusha.
-Ndugu
zangu ni wakati wa kutubu, Na toba zote tunatubu kwa MUNGU kupitia YESU
KRISTO pekee, hakuna njia nyingine ya kutubu. Warumi 10:9-10 '' Kwa
sababu, ukimkiri YESU kwa kinywa chako ya kuwa ni BWANA, na kuamini
moyoni mwako ya kuwa MUNGU alimfufua katika wafu, utaokoka. Kwa maana
kwa moyo mtu huamini hata kupata haki, na kwa kinywa hukiri hata kupata
wokovu. ''
-Wachawi tubuni
-Waongo tubuni.
-Wazinzi na waasherati tubuni.
-Wambea tubuni.
-Wasengenyaji tubuni.
-Mama na baba tubuni.
-Vijana na wazee tubuni.
-Watoto na mabinti tubuni.
-Ni saa ya kutubu.
Ndugu, tubu dhambi zako zote maana nimetaja 1% tu ya dhambi.
MUNGU hasa anataka kwanza toba ya kweli, Kujificha na kutenda wema
machoni pa watu hakutakusaidia ndugu. Mkimbilie BWANA YESU ili akuokoe.
''Kijapo kiburi ndipo ijapo aibu; Bali hekima hukaa na wanyenyekevu. -Mithali 11:2.
Wanyenyekevu ni wale wanaokubali kumpokea BWANA YESU na kutubu
Kwa sasa naishia hapo, MUNGU akitupa nafasi tutajifunza tena siku
nyingine.na kama hujampokea BWANA YESU muda wa kumpokea ni leo wala sio
kesho, amua leo na atakuandika jina lako katika kitabu cha uzima na
utaanza kuukulia wokovu kwa mafundisho kanisani. MUNGU ana makusudi
kabisa na wewe, hataki upotelee motoni anataka uende uzimani aliko KRISTO BWANA.
MUNGU akubariki sana
Saturday, 28 October 2017
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
KAZI KUU TANO (5) ZA IMANI KATIKA MAOMBI.
Bwana YESU atukuzwe ndugu zangu. Karibu tujifunze Neno la MUNGU. Uhusiano ni upendo unaozaa ushirikiano na mawasiliano kati ya pande m...
-
Bwana YESU atukuzwe ndugu zangu. Karibu tujifunze Neno la MUNGU. Uhusiano ni upendo unaozaa ushirikiano na mawasiliano kati ya pande m...
-
Bwana Yesu asifiwe… Imeandikwa ; “ Bali wote waliompokea aliwapa uwezo wa kufanyika watoto wa Mungu, ndio wale waliaminio jina lake; “Y...
-
Ni miaka mingi nimekuwa nikijiuliza swali hili, nitawezaje kumpenda Mungu kwa moyo wangu wote, kwa akili zangu zote na kwa nguvu zangu zote...
No comments:
Post a Comment