Toba ni nini na ni muhimu kwa ajili ya wokovu?"
Jibu:
Wengi huelewa neno toba kuwa na maana ya "kugeuka kutoka dhambi" Hii si
tafsiri ya Biblia ya toba. Katika Biblia, neno toba lina maana ya
"kubadili mawazo ya mtu." Biblia pia inatuambia kwamba toba ya kweli
itasababisha mabadiliko ya vitendo (Luka 3:8-14; Matendo 3:19). Matendo
26:20 inasema, "bali kwanza niliwahubiri wale wa Dameski na Yerusalemu,
na katika nchi yote ya Uyahudi, na watu wa Mataifa kwamba watubu na
kumwelekea Mungu, wakiyatenda matendo yanayopatana na kutubu kwao."
Ufafanuzi kamili wa Biblia wa toba ni badiliko la nia akilini ambayo
matokeo yake yamo katika matendo yaliyobadilika.
Basi, kuna uhusiano gani kati ya toba na wokovu? Kitabu cha Matendo
kinaonekana kuzingatia toba hasa inayo husu wokovu (Matendo 2:38; 3:19;
11:18; 17:30; 20:21; 26:20). Kutubu, kuhusiana na wokovu, ni kubadili
akili yako katika suala la Yesu Kristo. Katika mahubiri ya Petro siku ya
Pentekoste (Matendo 2), anamalizia na wito kwa watu watubu (Matendo
2:38). Tubu kutokana na nini? Petro anawaita watu walio mkataa Yesu
(Matendo 2:36 ) wabadili mawazo yao kumhusu, kutambua kwamba hakika Yeye
ni "Bwana na Kristo" (Matendo 2:36 ). Petro anawaita watu wabadili
mawazo yao kutoka kumkataa Kristo kama Masihi na kuwa na imani kwake
kama Masihi na mwokozi wetu.
Toba na imani inaweza kueleweka kama vile "pande mbili za sarafu moja."
Haiwezekani kuiweka imani yako katika Yesu Kristo kama mwokozi bila
kwanza kubadilisha mawazo yako kumhusu yeye na chenye amefanya. Hata
kama ni toba ya katao ya makusudi au toba ya kutojua au kutokua na haja,
ni badiliko la akili. Toba ya kibiblia, uhusiana na wokovu, ni
kubadilisha mawazo yako kutoka kwa kumkataa Kristo hadi kuwa na imani
katika Kristo.
Ni muhimu sana tuelewe kuwa toba si kazi sisi huifanya ili tupate
wokovu. Hakuna mtu anayeweza kutubu na kuja kwa Mungu, isipokuwa Mungu
amvute huyo mtu kwake (Yohana 6:44). Matendo 5:31 na 11:18 zinaonyesha
kwamba toba ni kitu ambacho Mungu anatoa - inawezekana tu kwa sababu ya
neema yake. Hakuna mtu anaweza kutubu, isipokuwa Mungu ampe toba. Wokovu
wote, ikiwa ni pamoja na toba na imani, ni matokeo ya Mungu kutuvuta
kwake, kuyafungua macho yetu, na kubadilisha mioyo yetu. Uvumilivu wa
Mungu hutuongoza sisi kutubu (2 Petro 3:9), kama ilivyo wema wake
(Warumi 2:4).
Huku toba ikiwa si kazi inayotuletea wokovu, toba kwa ajili ya wokovu
huishia katika matendo. Ni vigumu sana kubadili akili yako kikamilifu
bila ya kusababisha mabadiliko katika matendo. Katika Biblia, toba
matokeo yake ni mabadiliko ya tabia. Hiyo ndio sababu ni kwa nini Yohana
Mbatizaji aliwaita watu "kuzaa matunda yapasayo toba" (Mathayo 3:8).
Mtu ambaye kwa kweli ametubu kutoka kwa kumkataa Kristo hadi imani
katika Kristo atatoa ushahidi wa maisha yaliyobadilishwa (2 Wakorintho
5:17, Wagalatia 5:19-23; Yakobo 2:14-26). Toba, ikieleweka vizuri, ni
muhimu kwa wokovu. Toba ya kibiblia ni kubadilisha mawazo yako kuhusu
Yesu Kristo na kumgeukia Mungu katika imani kwa wokovu ( Matendo 3:19).
Kugeuka kutoka dhambi sio fafanuzi sahihi ya toba, lakini ni mojawapo ya
matokeo ya kweli, toba iliyoweka misingi yake katika kuelekea kwa Bwana
Yesu Kristo.
Saturday, 28 October 2017
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
KAZI KUU TANO (5) ZA IMANI KATIKA MAOMBI.
Bwana YESU atukuzwe ndugu zangu. Karibu tujifunze Neno la MUNGU. Uhusiano ni upendo unaozaa ushirikiano na mawasiliano kati ya pande m...
-
Bwana YESU atukuzwe ndugu zangu. Karibu tujifunze Neno la MUNGU. Uhusiano ni upendo unaozaa ushirikiano na mawasiliano kati ya pande m...
-
Bwana Yesu asifiwe… Imeandikwa ; “ Bali wote waliompokea aliwapa uwezo wa kufanyika watoto wa Mungu, ndio wale waliaminio jina lake; “Y...
-
Ni miaka mingi nimekuwa nikijiuliza swali hili, nitawezaje kumpenda Mungu kwa moyo wangu wote, kwa akili zangu zote na kwa nguvu zangu zote...
No comments:
Post a Comment