Saturday, 3 November 2018

SOMO LA MADHABAHU (KUNA MAENEO MATANO).

                                     

1.    Namna ya kufahamu madhabahu,
2.    Mambo yanayotendeka kwenye madhabahu ya shetani,
3.    Makusudi Mungu kuwa na madhabahu,
4.    Ili tuweze kumuona Mungu katika maisha ni lazima tumjengee Mungu madhabahu,
5.    Namna ya kumjengea Mungu madhabahu.

1.    NAMNA YA KUFAHAMU MADHABAHU
•    Ni jambo la muhimu kwa muombezi  kufahamu mambo yanayo fanyika katika madhabahu.

•    Madhabahu ni nini?
Madhabahu ni mahali pa juu palipoinuka pa kutolea dhabihu(zamani),watu walijenga madhabahu wakachinja wanyama na kuwateketeza juu ya hiyo madhabahu.
•    Madhabahu ni mahali popote mtu anapokutana na Roho, inaweza kuwa roho ya Mungu au ya shetani.
•    Shetani ameiga mambo mengi ya Mungu, misingi ambayo Mungu anaitumia ndiyo hiyohiyo  shetani anaitumia.
•    Kutoka 20: 24 Madhabahu inayojengwa kwa ajili ya Mungu Mungu anakuja na kukubarikia, Madhabahu inayojengwa  kwa ajili ya shetani inatumika kwa ajili yake, Madhabahu inayojengwa na shetani  inaleta laana.
•    Madhabahu ya Mungu inaleta Baraka.
•    Mungu alipomuumba mwanadamu alimfundisha juu ya kufanya madhabahu (kujenga) wakati ule wa Kaini na Abeli  Mwanzo  4: 1-5
•    Mwanzo 8: 15-22 Nuhu alivyotoka kwenye safina jambo la kwanza alimjengea Mungu  madhabahu. Akamtolea Mungu dhabihu kwenye madhabahu hiyo aliyo ijenga,
•    MSTARI wa 21 Bwana  akasikia harufu iliyompendeza toka kwenye madhabahu.
•    Mwanzo 9: 8-17 Bwana anajibu kwa sababu ya madhabahu ya Nuhu aliyoijenga. Hata leo tunayo majibu ya kutokana na madhabahu aliyo ijenga Nuhu. Kuna wakati wa kupanda na kuna wakati wa kuvuna, wakati wa mvua na wakati wa kiangazi.
•    Na tunapouona upinde tunakumbuka agano la Mungu na wanadamu.
•    Penye madhabahu ni mahali pa maagano,
•    Kutoka 17: 15-16 Musa alijenga madhabahu baada ya vita vya Joshua.
•    Hesabu 23: 14 Balamu alijenga madhabahu saba kutaka mawasiliano na Roho ya Mungu ailaani Israel, Mungu akasema hawezi kuwalaani Israel.
•    Wakati  umefika wa  sisi kutamka  maneno na kumjengea Mungu madhabahu.
•    Kuna madhabahu zinazotawala katika nchi hii ambazo shetani amezijenga.
•    Siku zimefika kujua madhabahu zilizopo katika nchi yetu na kuziharibu,kuvunja kila makubaliano na maagano yaliyofanyika.
•    Yer.  1:10
•    Kama usipoinua madhabahu na kumwinua yesu katika mji shetani  ataendelea kukandamiza.
•    Simama katika mji wako na mtaa wako toa tangazo mwambie Mimi……………………najua wewe shetani  unatawala  katika mji huu nina
Kutangazia  kuanzia leo hii katika jina la Yesu Kristo shetani  na kila kitu chako uondoke.
•    Anza kwa kuomba msamaha kwa Mungu kwa kuzembea na kutoa nafasi kwa shetani kutawala mtaa huu.
•    Simama  kinyume na kila dhabihu iliyofanyika katika mtaa huu na kuikataa katika jina la
Yesu na kuiondoka nakuiharibu katika jina la Yesu Kristo wa Nazareti.
•    Luka 11: 1-4 Wanafunzi  wanamwambia  Yesu  utufundishe  kuomba. Hili ndilo andiko
Linalotufundisha kuomba.
•    Tunaposema Baba yetu,tunaweka uhusiano kati ya baba na motto. Tunapaswa kukumbuka Mungu ana ufalme duniani.
•    Zaburi 24: 1 Nchi na vyote viijazavyo ni mali ya Bwana, Dunia na wote wakaao ndani yake.
•    Maombi  yanapaswa kutumika kuleta ufalme wa Mungu ulimwenguni lazima tuutafute ufalme wa Mungu ulimwenguni .
•    Warumi 12: 1-2 Kuitoa miili yetu kuwa dhabihu hata katika kufikiri kwetu na kubadilisha ili tujue mapenzi ya Mungu kwetu.
•    Ni lazima tuyatoe maisha yetu na kufanywa upya nia zetu. Sisi tutafute kujua mapenzi ya Mungu kwetu.
Tunapomtafuta ndipo Mungu anafunua mapenzi yake kwetu.
•    Na tunapojua hivyo hata maombi yetu hayatakuwa magumu sana kwetu.
•    Maombi ndiyo kodi ambayo  Mungu anayatumia kutumia bajeti yake.
•    Ufunuo 8: 1-5 Madhabahu inawakilisha kile kiti cha Enzi cha Mungu. Na kuona malaika wanaangalia na kupokea maombi, kile kilichomo ndani yake wanamimina katika dunia.
•    Hakuna  kitu kinachofanyika duniani ila ni maombi na uvumba toka kwa Mungu.
Ezekieli 22: 30 Mungu anamtafuta mtu duniani ampelekee maombi.
•    Ufunuo 5: 8-10 kuna wazee 24wanaokaa katika kiti cha Enzi na kuweka maombi ya watakatifu. Maombi ya watakatifu ni muhimu sana.
•    Ufunuo 1: 5-6 Yesu alikufa ili kutufanya sisi wafalme na Makuhani
Wafalme tumiliki katika nchi,
Makuhani  tumiliki katika madhabahu yake.
•    Mathayo 5: 8 Heri wenye moyo safi maana hao watamwona Mungu. Mungu anataka tuwe na moyo safi, Haki yetu izidi ile ya mafarisayo ili tuweze kumuona Mungu.
•    Makusudi ya moyo wako Mungu ayajue, usafi wa moyo wako ni muhimu sana
•    Galatia 5: 25 Tukiishi kwa Roho na tuenende kwa roho.
•    Uthamani na jinsi unavyo ufikiria ufalme wa (Mbinguni) wa Mungu ni wa thamani sana kwako. Je! Ufalme wa Mungu una thamani gani kwako?

No comments:

Post a Comment

KAZI KUU TANO (5) ZA IMANI KATIKA MAOMBI.

Bwana YESU atukuzwe ndugu zangu. Karibu tujifunze Neno la MUNGU. Uhusiano ni upendo unaozaa ushirikiano na mawasiliano kati ya pande m...