Thursday, 8 November 2018

Katika maisha yako uko ukurasa wa ngapi?



Katika maisha yako uko ukurasa wa ngapi?
 Je uko ukurasa wa pili wa maisha yako?
 Je uko ukurasa wa katikati wa maisha yako?
 Je uko ukurasa wa pili kutoka mwisho wa kuishi kwako?
 Je uko ukurasa wa mwisho wa kuishi kwako?
 Ndugu uko ukurasa wa ngapi wa maisha yako?
Ndugu, haijalishi uko ukurasa wa ngapi wa maisha yako ila muhimu sasa tena Leo ni wewe kumpokea YESU KRISTO kama Mwokozi wako na kuanza kuishi maisha matakatifu.
Kama umeshampokea YESU kama Mwokozi wako binafsi basi hakikisha unaishi maisha matakatifu kama yeye YESU anavyokuagiza kupitia Biblia takatifu.
Anza sasa kuishi maisha matakatifu ya Wokovu kama wewe ulikuwa unaigiza tu katika Kanisa.
Kumbuka mtu ana hatua kuu tatu za kupitia, mtu anazaliwa, anaishi kisha anakufa.
Ndugu itumie Leo yako kutengeneza na YESU Mwokozi.
Ishi maisha matakatifu katika KRISTO YESU ili hata ukurasa wako Ukifungwa hata kama ni Leo wewe utaenda uzima wa milele.
Ujumbe kama huu huwa haujileti tu wenyewe bali ROHO MTAKATIFU anaufunua.
YESU anakungoja kwenye lango la kuingia mbinguni, na lango hilo liko moja tu.
Ukilifanya Kanisa kuwa kichaka chako cha kuficha uovu shauri yako, kama unaona ni sawa tu kuendelea na uzinzi na uasherati shauri yako, kama umeng'ang'ania dini ya baba yako lakini haikupeleki mbinguni shauri yako.
Kama hutaki kuokoka shauri yako.
Bwana YESU kwa huruma na upendo sana anasema mbele za watu wote ukiwemo na wewe kwamba " mimi nalikuja ili wawe na uzima, kisha wawe nao tele.-Yohana 10:10"
MUNGU akubariki Sana.

No comments:

Post a Comment

KAZI KUU TANO (5) ZA IMANI KATIKA MAOMBI.

Bwana YESU atukuzwe ndugu zangu. Karibu tujifunze Neno la MUNGU. Uhusiano ni upendo unaozaa ushirikiano na mawasiliano kati ya pande m...