Tuesday, 30 October 2018

SIRI YA MAFANIKIO KWA MWANADAMU

Maisha ya watu wengi yamekwama na hata wale wanaojidhania kuwa wamebarikiwa wanashindwa kufikia viwango vikubwa vya mafanikio ambayo MUNGU anayakusudia kwao kwa sababu ya tatizo la kupenda kujikusanyia na kusahau kujitoa kuwa BARAKA kwa wengine.
Mfumo wa maisha umewekwa katika kutoa na  kupokea, ili uishi lazima kupumua na huwezi kupumua kwa kuvuta pumzi ndani peke yake bila KUTOA NJE, UTAKUFA. Maji yenye uhai ni yale yanayopokea na kutoa, maji yakituama yaani hayatoi lazima yatoe harufu mbaya kwa sababu hayana uhai.
Na unapofika hatua umebarikiwa na MUNGU na unageuka kuwa mkusanyaji tu, unataguta fursa za kupokea na kukusanya bila kutafuta fursa za kutoa na kuboresha maisha ya wengine, unafungulia mlango roho ya Ukengeufu, lazima utaiacha njia ya MUNGU. Muangalie Mfalme Suleiman utoaji ulimpa Neema na kibali kwa Mungu (1 Wafalme 8:62-65) alipobadilika na kuwa mkusanyaji tu akamuasi Mungu na kuabudu miungu mingine (1 Wafalme 11:4). Mtume Paulo anatukumbusha, "Katika mambo yote nimewaonyesha ya kuwa kwa kushika kazi hivi imewapasa kuwasaidia wanyonge, na kuyakumbuka maneno ya Bwana Yesu, jinsi alivyosema mwenyewe, NI HERI/BARAKA/(KUNA UTOSHELEVU KATIKA) KUTOA KULIKO KUPOKEA. (Matendo 20:35KJV)
Mungu anamwambia Ibrahimu maneno haya;
Nami nitakufanya wewe kuwa TAIFA KUBWA, NA KUKUBARIKI, na kulikuza jina lako; NAWE UWE BARAKA;
(Mwanzo 12:2)
Na Mungu akatimiza ahadi yake katika Mwanzo 13:2. Naye Abramu alikuwa ni tajiri sana kwa mifugo, kwa fedha, na dhahabu." Lakini hakufanywa tajiri sana kwaajili yake tu na watoto wake kwani alimbiwa anabarikiwa ili awe BARAKA. Pia atafanywa kuwa taifa kubwa.TAIFA KUBWA MAANA YAKE UTATEGEMEWA NA WATU WENGI. Neno hili linakuja kutimia katika (Mwanzo 14:14) "Abramu aliposikia ya kwamba nduguye ametekwa mateka, akawapa silaha VIJANA WAKE (WATUMISHI AU WATUMWA), WALIOZALIWA KATIKA NYUMBA YAKE, watu WATU MIA TATU KUMI NA WANANANE (318), akawafuata mpaka Dani." KUSUDI LA MUNGU KUKUBARIKI LA KWANZA KABISA NI ILI ATUMIE HIZO BARAKA KUBARIKI WENGINE. UNAPOACHA KUTOA UNAKATA NEEMA YA ONGEZEKO KWENYE MAISHA YAKO. HATA KAMA UNA HALI NGUMU NAMNA GANI SIKU ZOTE TAFUTA NAFASI YA KUWA BARAKA KWA MTU MWINGINE.

No comments:

Post a Comment

KAZI KUU TANO (5) ZA IMANI KATIKA MAOMBI.

Bwana YESU atukuzwe ndugu zangu. Karibu tujifunze Neno la MUNGU. Uhusiano ni upendo unaozaa ushirikiano na mawasiliano kati ya pande m...