Tuesday, 23 October 2018
KINYWA CHA MTUMISHI WA MUNGU KILIVYO.
1. Kinatakiwa kuhifadhi maarifa ya Neno la MUNGU.
Maana yeye huyo mtumishi ni mjumbe wa MUNGU.
Malaki 2:7 na Yeremia 1:9
2. Kinahubiri habari njema za ufalme wa MUNGU, kuwaganga waliovunjika moyo na kuwatangazia Uhuru wao wale waliofungwa kiroho.
Yaani kinahubiri injili ya YESU KRISTO iokoayo.
Isaya 61:1, Mathayo 10:8 na Isaya 35:4
3. Kinawaambia watu makosa yao, dhambi zao na uovu wao ili waache, watubu na watengeneze na MUNGU kupitia KRISTO YESU.
Isaya 58:1, Ufunuo 3:19 na 2 Timotheo 4:2
4. Kinamsikiliza ROHO MTAKATIFU na kumtii.
Yohana 14:26, Matendo 13:2 na 1 Kor 2:10
5. Kinatengeneza mahali palipokuwa pameharibika.
Ezekieli 22:30.
Ujumbe huu ni ufunuo nilipewa na ROHO MTAKATIFU.
Siku moja nitafafanua somo hili.
Je wewe ni Mtumishi hai wa MUNGU katika KRISTO YESU?
Kama ni kweli naamini kuna kitu umejifunza na pitia maandiko hayo.
MUNGU akubariki Sana
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
KAZI KUU TANO (5) ZA IMANI KATIKA MAOMBI.
Bwana YESU atukuzwe ndugu zangu. Karibu tujifunze Neno la MUNGU. Uhusiano ni upendo unaozaa ushirikiano na mawasiliano kati ya pande m...
-
Bwana YESU atukuzwe ndugu zangu. Karibu tujifunze Neno la MUNGU. Uhusiano ni upendo unaozaa ushirikiano na mawasiliano kati ya pande m...
-
Bwana Yesu asifiwe… Imeandikwa ; “ Bali wote waliompokea aliwapa uwezo wa kufanyika watoto wa Mungu, ndio wale waliaminio jina lake; “Y...
-
Ni miaka mingi nimekuwa nikijiuliza swali hili, nitawezaje kumpenda Mungu kwa moyo wangu wote, kwa akili zangu zote na kwa nguvu zangu zote...

No comments:
Post a Comment