Monday, 22 October 2018

AHADI ZA MUNGU ZINAPOTUJARIBU


Bwana Yesu atukuzwe mpendwa wangu.
Kwa ufunuo wa Roho Mtakatifu mtunga Zaburi anafunuliwa na kuandika yale yaliyompata mtumishi wa Mungu Nabii Yusufu mwana wa Yakobo.
Anafunuliwa na kuandika:
Mungu "Akaiita njaa iijilie nchi, Akakiharibu chakula chote walichokitegemea.
Alimpeleka mtu mbele yao, Yusufu aliuzwa utumwani.
Walimwumiza miguu yake kwa pingu, Akatiwa katika minyororo ya chuma.
Hata wakati wa kuwadia neno lake, Ahadi ya Bwana ilimjaribu.
Mfalme alituma watu akamfungua, Mkuu wa watu akamwachia.
Akamweka kuwa bwana wa nyumba yake, Na mwenye amri juu ya mali zake zote.
Awafunge masheki wake kama apendavyo, Na kuwafundisha wazee wake hekima.
Israeli naye akaingia Misri, Yakobo akawa mgeni katika nchi ya Hamu.
Akawajalia watu wake wazae sana, Akawafanya kuwa hodari kuliko watesi wao.
Akawageuza moyo wawachukie watu wake, Wakawatendea hila watumishi wake" #Zaburi 105:16-25
Utimilifu wa ahadi ya Mungu juu ya maisha yetu huambatana na mitihani kuzipima imani zetu kama tuko thabiti ama la.
Ibrahimu utimilifu wa ahadi ya Mungu juu yake ulipotimia alijaribiwa hata akaambiwa amtoe sadaka mwanawe wa pekee aliyemsotea kwa kumsubiri kwa miaka mingi sana. Ibrahimu alishinda.
Si kila wakati tunaweza kushinda lakini Mungu wa neema huendelea kuzipima imani zetu aone namna gani tunajitoa dhabiti kumtegemea yeye.
Nabii Yusufu yalimkuta pia. Ahadi ambazo Mungu alizungumza naye akiwa kijana mdogo sana kwamba atamfanya kuwa mtu mkuu ilipokaribia kutimia alijaribiwa kwa majaribu makuu.
Kwanza kwa kutenganishwa na familia yake hata akauzwa utumwani. Kama haitoshi akiwa utumwani Bwana aliendelea kuwa pamoja naye. Natamani sana Mungu atupe mioyo ya subira kumtumaini Mungu kila tupitapo.
Nabii Yusufu alifungwa na utimilifu wa ahadi ya Mungu uliendelea kumfuata huko huko gerezani na Mungu akatimiza ahadi yake.
Mwana wa Mungu nakuombea Bwana akupe neema ya kustahimili upitapo katika mitihani. Neema ya Mungu ikufunike ahadi zake zinapokujaribu. Hivyo ndivyo Bwana hufanya, ahadi zake hutujaribu ili atuone kama tuko thabiti katika imani.
Barikiwa

Image may contain: text

No comments:

Post a Comment

KAZI KUU TANO (5) ZA IMANI KATIKA MAOMBI.

Bwana YESU atukuzwe ndugu zangu. Karibu tujifunze Neno la MUNGU. Uhusiano ni upendo unaozaa ushirikiano na mawasiliano kati ya pande m...