Tuesday, 17 July 2018

NAKUOMBA NDUGU USIWE MJINGA


“Kwa hiyo iweni waangalifu jinsi mnavyoenenda, si kama watu wasio na hekima, bali kama wenye hekima, mkiukomboa wakati, kwa sababu nyakati hizi ni za uovu. Kwa hiyo msiwe wajinga, bali mpate kujua nini yaliyo mapenzi ya Bwana. Pia msilewe kwa mvivyo, ambamo ndani yake mna upotovu, bali mjazwe Roho. Msemezane ninyi kwa ninyi kwa zaburi, nyimbo na tenzi za rohoni, mkimwimbia na kumsifu Bwana mioyoni mwenu, sikuzote mkimshukuru Mungu Baba katika Jina la Bwana wetu Yesu Kristo kwa kila jambo. Nyenyekeaneni ninyi kwa ninyi kwa heshima kwa ajili ya Kristo” #Waefeso 5:15-21
Nakusalimu katika jina la Yesu mpendwa wangu. Ujumbe huu wa kinabii alhamisi ya leo hauna lengo la kutaka kuingilia uhuru wa kunywa kwako vinywaji. Lakini lengo halisi Mungu anataka kutusaidia kujua neema ya nguvu ndani yetu inavyoweza kutusaidia kushinda dhambi.
Najua tuna maoni tofauti tofauti sana kuhusu unywaji wa vileo. Na nikupe tu changamoto usiwe mwepesi wa kuingilia uhuru wa watu katika unywaji. Msimamo wa kiBiblia uko wazi.
“Yeye aliye dhaifu wa imani, mkaribisheni, walakini msimhukumu mawazo yake. Mtu mmoja anayo imani, anakula vyote; lakini yeye aliye dhaifu hula mboga. Yeye alaye asimdharau huyo asiyekula, wala yeye asiyekula asimhukumu huyo alaye; kwa maana Mungu amemkubali. Wewe u nani unayemhukumu mtumishi wa mwingine? Kwa bwana wake mwenyewe yeye husimama au huanguka. Naam, atasimamishwa, kwa kuwa Bwana aweza kumsimamisha.”#Warumi 14:1-4
Kwa hyo kwa habari ya kula nakunywa mie sikuingilii maana imeandikwa:
“Vitu vyote ni halali kwangu, lakini si vyote vifaavyo; vitu vyote ni halali kwangu, lakini mimi sitatiwa chini ya uwezo wa kitu cho chote. Vyakula ni kwa tumbo, na tumbo ni kwa vyakula; lakini Mungu atavitowesha vyote viwili, tumbo na vyakula” #1Kor. 6:12
Nami wala siko tayari kutiwa chini ya mtu yeyote kuhusu kula nakunywa. Ni muhimu sana ukawa na msimamo wako binafsi.
Msimamo wa Mungu uko wazi kwamba ulevi ni dhambi. “Au hamjui ya kuwa wadhalimu hawataurithi ufalme wa Mungu? Msidanganyike; waasherati hawataurithi ufalme wa Mungu, wala waabudu sanamu, wala wazinzi, wala wafiraji, wala walawiti, wala wevi, wala watamanio, wala WALEVI, wala watukanaji, wala wanyang'anyi. Na baadhi yenu mlikuwa watu wa namna hii; lakini mlioshwa, lakini mlitakaswa, lakini mlihesabiwa haki katika jina la Bwana Yesu Kristo, na katika Roho wa Mungu wetu.” #1Kor. 6:9-11
Lengo halisi la ujumbe huu wa kinabii leo ni kwamba Bwana anakutaka mimi na wewe tusiwe wajinga tena katika mienendo yetu. Tunaishi katika zama za uovu, nasi tunaolikiri jina la Yesu hatupaswi kuishi katika uovu huo.
“"Maana wakati wa maisha yetu uliopita watosha kwa kutenda mapenzi ya Mataifa; kuenenda katika ufisadi, na tamaa, na ulevi, na karamu za ulafi, na vileo, na ibada ya sanamu isiyo halali"
#1Petro 4:3
Mpendwa wangu ni muda gani tupewe kuyatenda mapenzi ya Shetani? Nadhani yatosha muda tulioutumia kuyatenda mapenzi ya dunia. Huu ni muda mzuri wa kumtumikia Mungu na kuyatenda mapenzi yake.
Hakika hatupaswi kuendelea kuwa wajinga kwa kuendelea kuishi maisha ya uovu.
“Naam, tukiujua wakati, kwamba saa ya kuamka katika usingizi imekwisha kuwadia; kwa maana sasa wokovu wetu u karibu nasi kuliko tulipoanza kuamini - Usiku umeendelea sana, mchana umekaribia, basi na tuyavue matendo ya giza, na kuzivaa silaha za nuru. Kama ilivyohusika na mchana na tuenende kwa adabu; si kwa ulafi na ulevi, si kwa ufisadi na uasherati, si kwa ugomvi na wivu. Bali mvaeni Bwana Yesu Kristo, wala msiuangalie mwili, hata kuwasha tamaa zake” #Warumi 13:11-14
Mwenye masikio na asikie na Mungu aliye hai akubariki.
Neema ya Bwana wetu Yesu Kristo iwe pamoja nawe mwana wa Mungu na ikiwa umebarikiwa basi share ujumbe huu kwa mwingine naye abarikiwe
“YASIYOWEZEKANA KWA WANADAMU, YAWEZEKANA KWA MUNGU” #LUKA 18:27
Kwa maombezi, unataka kupokea uponyaji au kufunguliwa kwenye kifungo chochote kile, ushauri au unatamani ujitoe kikamilifu kumtumikia MUNGU na UNATAKA KUMPOKEA BWANA YESU AWE BWANA NA MWOKOZI WA MAISHA YAKO NA AKUSAMEHE DHAMBI ABADILISHE MAISHA YAKO NA TABIA MBAYA ZILIZOKUSHINDA basi wasiliana nasi kwa msaada wa Roho Mtakatifu tukusaidie +255 758 443 873. Ukipiga simu isipopokelewa tafadhali acha sms

No comments:

Post a Comment

KAZI KUU TANO (5) ZA IMANI KATIKA MAOMBI.

Bwana YESU atukuzwe ndugu zangu. Karibu tujifunze Neno la MUNGU. Uhusiano ni upendo unaozaa ushirikiano na mawasiliano kati ya pande m...