Monday, 30 July 2018

KAMA UMERIDHIKA DUNIA HII BORA UFE LEO.

"IF YOU DON'T HAVE AMBITION YOU SHOULDN'T BE ALIVE"

("KAMA WEWE NI MTU WA KURIDHIKA KIRAHISI NA ULICHONACHO HUPASWI KUWA HAI")

Ijumaa saa nne asubuhi.
Mwezi October 2011. Naendesha gari kuelekea Bagamoyo. Njiani naburidika na sauti za waimbaji wa Hillsong na wimbo wao

"LET THE PEACE OF GOD REIGN".

Aisee.
Bonge moja la wimbo. (Utafute kama hujawahi kuusikia utaniambia...)

So.. Huku nikiwaza mambo makubwa yaliyoko mbele yangu baada ya kuanza maisha ya ujasiriamali. Na pia hapo nikiwa ninawaza mambo niliyojifunza katika ujasiriamali so far. Nawaza  hatua niliyoanza kupiga. Nawaza maisha yangu ya miaka mingi ijayo na wale Mungu atakaonipa.

Hapo ni mwaka mmoja toka niache kazi yangu ya kuajiriwa Stanbic Bank Headquarters, Dar es Salaam. Jengo zuri sana pale Kinondoni limezungukwa na ofisi za ubalozi wa Ufaransa, apartments za Holiday Homes, Ubalozi wa Urusi na makazi ya balozi wa Uingereza. Aisee mahali pazuri hakika. Kazi nzuri ambayo niliipenda sana. Watu wazuri niliowapenda mno. Hasa my boss ambaye alinifundisha kuzingatia wajibu wangu everyday. Na wengine wengi walionifanya nione furaha kwenda kazini everyday. Ikiwa kazi yangu ya kwanza ya kuajiriwa baada ya masomo yangu ya Chuo Kikuu (na of course ya mwisho pia) niliifanya kwa miaka miwili tu nikaamua kuacha na kuingia kwenye ujasiriamali. Uamuzi ambao ulileta changamoto nyingi kwenye maisha yangu. Nyingi tu. Lakini pia ni uamuzi ulionifungua na kunipeleka nilikotaka kuelekea kimaisha.. Na uamuzi ambao umenifungulia milango ambayo sikuwahi kujua kama ipo.

Nikaacha kazi Stanbic na kwenda kuuza Popcorn Mwenge wakati ule stendi ya daladala haijahamishiwa Makumbusho. Nakumbuka jinsi watu wengi waliokuwa wakinijua walivyohisi nimechanganyikiwa. Kutoka bank headquarters kwenye kiyoyozi na kwenda kusimama stendi ya daladala kwenye kelele na lugha za mtaani unaenda kuuza bisi! Maana nikisema popcorn unaweza kuwaza kama za kwenye movie theatre zile.  Ni bisi ndiyo . Hahaaa. I remember binti mmoja tulimaliza naye Chuo Kikuu na alikuwa serikalini wakati ule alinikuta nauza bisi akashangaa kweli nadhani alikuwa anajiuliza moyoni: "WHAT HAPPENED TO THIS GUY?"
Unajua ukiangalia macho ya mtu unaweza kujua anajiuliza nini..

And countless other people ambao walizoea kuniona nimevaa suti sasa wanakutana na mimi nimebeba mahindi ya popcorn na T-shirt na jeans.
Ukiwa Benki na unavaa suti unanukia perfume kali na kiyoyozi ukikutana na marafiki wanaku-hug automatically. Ukiwa na harufu ya bisi hakuna anayetaka kuku-hug. Nani anuke bisi. Atakayekuhug hivyo hivyo una harufu ya bisi huyo ni malaika. Trust me.

So nilipoteza marafiki wengi sana.
Na ndugu.
Na nikapata marafiki wapya wengi.
Na ndugu wapya.

Hayo yote yananijia nikiwa naendelea na safari yangu kwenda Bagamoyo ijumaa hii October 2011.
Nawaza niliowaacha Stanbic. Wana mshahara mzuri bado. Wanavaa suti nzuri bado. Wanakula vizuri bado. Wako jengo zuri bado. Kichwani linakuja swali ghafla: "BUT WHY DID YOU LEAVE THAT PLACE ANDREA?"

And then kichwani linakuja jibu immediately: BECAUSE OF MY AMBITION.

Yes. Kwa sababu sikuridhika na hatua hiyo nilitaka makubwa zaidi.

Swali jingine likaja: "Sasa si ungeenda Benki nyingine kubwa zaidi?" Jibu likaja: HAKUNA BENKI KUBWA KWA MWAJIRIWA.

Nikasmile.
Nikajikuta nadandia chorus ya wimbo kwenye gari..

"Oh Lord, I hunger for more of You
Rise up within me, let me know Your Truth
Oh Holy Spirit, saturate my soul
And let the life of God, fill me now
Let Your Healing power
Breath life and make me whole
And let the peace of God
Let it reign."

Aisee hebu Ingia YouTube baadaye usikilize hii kitu utanielewa....

:::::::::::::::::::::::::::::::::::::

So...
Nimekumbuka jambo hili baada ya kuwaza kuwa nimejishughulisha na ujasiriamali kuanzia chini sana kwa miaka 7 sasa mpaka nimefika mahali pa kuweza kumshauri mwingine kuhusu ujasiriamali na biashara baada ya hatua niliyopiga. Nimefika mahali pa watu kuuliza kama nina vitabu wanunue. Nimefika mahali pa watu kuniita na kunilipa ili niwachangie mawazo niliyonayo.

Japo bado hiyo ni hatua ya chini ukilinganisha na nilichoazimia kutimiza duniani lakini imenifanya kukumbuka nilikoanzia. Nikaona niseme kitu kuhusu watu waliofanikiwa huenda kikakusaidia katika safari yako ya mafanikio.

Ni hivi: Usiridhike na hali yoyote kiuchumi maishani mwako!

Nimekuwa na kawaida ya kununua na kusoma majarida ya Forbes toka mwaka 2012 kujifunza kuhusu watu waliofanikiwa kiuchumi walianzia wapi na nimegundua kuwa wala usiwaze walipoanzia maana huenda wewe usiweze. Wengi wameanzia CHINI sana.

Lakini cha kushangaza ni kuwa wengi wao WALIAMUA kwa makusudi kuanza chini baada ya kuwa maisha yao yamefikia mahali ambapo binadamu wa kawaida angeweza kuridhika na maisha yakasonga tena vizuri sana.

Kwamba mtu amezaliwa familia bora ya kitajiri badala ya kuridhika tu na "kula bata" lakini anahangaika kuliko waliomtangulia.

Ama mtu ana kazi nzuri  mshahara mzuri na maisha ambayo wengi wanayatamani halafu anayaacha. Anaanza kitu kingine tena chini kabisa mahali pa kuchekwa.
ANADIRIKI kuwa kituko.

Ngoja nikupe mfano hai. Fikiria una ndugu yako. Amesoma vizuri hapa nchini japo kwa ada ya kuunga kwa wazazi ambao ni wakulima. Lakini bahati nzuri anapata SCHOLARSHIP kwenda kusoma Ulaya. Anaenda. Mnafurahi. Miaka inaenda. Mingi. Kamaliza masomo yake ya juu  huko huko. Kapata kazi nzuri huko. Kampuni ya kigeni. Analipwa vizuri si mbaya sana. Baadaye anaomba arudi Tanzania. Anakubaliwa na anaanza kazi katika kampuni hiyo jijini Dar es Salaam. Anafanya kazi kama mfanyakazi wa kawaida. Lakini anapanda vyeo kidogo kidogo hadi yeye ndo anakuwa TOP! Boss wa juu kabisa. Mnajua sasa Mungu amewaona na nyinyi. Mmepata MTU KATIKA WATU.

Ghafla anaacha kazi akiwa top. Anaacha. Halafu anaamua kurudi kijijini kwenu halafu anaanza kuwa mchuuzi wa kalamu za wino!

Wewe utamfikiriaje mtu huyo?

Amechanganyikiwa? Amerogwa?

And yet hiyo ndo story ya Reginald Mengi. Nilipoiona story hiyo kwenye jarida la Forbes mwanzoni mwa mwaka 2014 nilimheshimu sana huyu mzee. Na niliheshimu zaidi maamuzi niliyoyafanya pia miaka kadhaa nyuma sasa yapata miaka 7 iliyopita!

Vijana wengi wako Chuo wanaotamani kuajiriwa kampuni kubwa kama PWC leo.
Siyo kuwa partners. No. Kuajiriwa tu. Mpaka wanamlilia Mungu awape hiyo fursa. Lakini Mengi alidiriki kuondoka PWC akiwa Managing Partner na Chairman. Akaacha hela nzuri nyumba ya kampuni na gari zuri nk na kwenda kuuza kalamu.

Why?

Jibu ni moja tu: AMBITION.

Ambition ya kusaidia watu. Ambition ya kuacha alama duniani. Ambition ya ku-inspire wengine...Nk.

Unaweza kuuliza kuwa kwani mtu ukiwa kwenye ajira huwezi kuacha alama hadi uache ajira?

Well hakuna anayekwambia kuacha kitu.
Mengi HAKUAMBIWA na mtu.
Bill Gates HAKUAMBIWA aache Havard.

Binafsi sikuambiwa na mtu kuwa niache kazi.

No one is telling you to leave anything.
Hivi vitu si vya kuambiwa. Vinatokea NDANI.

Na huwezi kuelewa maamuzi ya aina hiyo mpaka siku utakayoelewa kauli hii aliyowahi kuitoa bwana Aliko Dangote. Tajiri namba moja mweusi duniani kwamba:

"IF YOU DON'T HAVE AMBITION YOU SHOULDN'T BE ALIVE!"

Mara ya kwanza nilipoiona kauli hii nikiwa tayari kwenye ujasiriamali niliwaza sana. Nikasema hivi huyu jamaa ana maana gani kusema KAMA UMERIDHIKA NA HATUA ULIYOPO MAISHANI BASI HUPASWI KUWA HAI?

Lakini kadri ninavyokutana na watu hasa wanaotamani kufanikiwa kiuchumi na kuona wanavyoishi na wanavyowaza ndivyo ninavyozidi kuelewa kauli ya Alhaji Dangote!

Leo hii watu hawaelewi  kwa nini Mengi bado anatunga kitabu iwe njia nyingine ya mapato yake mapya maisha yake yote! Mbona ana pesa tayari? Haridhiki tu?

Ukiona unajiuliza hivyo ujue you don't have ambition na ndo Dangote anasema hupaswi kuwa hai wewe.

Unajiuliza Diamond bado anatunga nyimbo ili iweje. Anafungua biashara nyingine ili iweje. Hakuridhika kuimba na DAVIDO na P-SQUARE na NEYO?

AMBITION.

Anajua waliomtangulia waliimba vizuri lakini walikosa AMBITION. Waliridhika kuwa maarufu na sasa "WAMEKUFA". Waliosurvive ni ambao hawakuridhika na pale walipokuwa wamefika.

Kitakachokufanya na wewe "usife kiuchumi" na kwenye mioyo ya watu ni AMBITION. Ukikosa AMBITION you are committing suicide my friend.
You die!

Jiulize Ronaldo na Messi kwa nini wanalia kukosa kombe la dunia mbona ndo wanaongoza kwa pesa katika football wanalia nini sasa?

Jibu ni WANA AMBITION. HAWAJARIDHIKA.
Angalia tatizo la taifa lisilo na AMBITION tukipata mchezaji mmoja kucheza Ulaya tunaridhika. Siku Taifa Stars ikiifunga Brazil itakuwa sherehe.

According to FIFA RANKINGS za tarehe 7 June mwaka huu. Brazil ni number 2 after Germany.. Uingereza ilikuwa namba 12. Na nchi ya kwanza kwa Africa Tunisia ikiwa namba 21 na Tanzania ni namba 140 katika nchi 200+ za FIFA.
Rankings mpya zitatoka tarehe 19 July baada ya kombe la dunia.

Yani nchi bora bara zima la Africa ukiipeleka kidunia inashika namba 21. Never number 1. Why?

Little or no ambition.

Tajiri namba moja kwa watu weusi wooote duniani ukimpeleka kidunia ni namba 100. Aliko Dangote. Huoni kwa nini weupe  wanatudharau?
Huoni kwa nini Dangote ana hasira ya kuongeza miradi kila leo?
Umeelewa kwa nini Bakhresa hajaridhika?

Halafu wewe UMERIDHIKA

Unajiuliza eti sasa na wao wana  tamaa tu. Hela zote hizo?🤣🤣

Ukiona unawaza hivyo ujue uko hai kibahati tu any time unapotea maana hutaki kuleta impact. Ila upo tu duniani hujui kwa nini bado upo.

Unajiuliza Jeff Bezos mmoja tu ndani ya utajiri wake wa sasa kuna utajiri wa Bill Gates ($90 billion) plus wa Dangote $12 billion) plus wa matajiri wote wakubwa wa Tanzania, Kenya na Uganda kwa pamoja. Na bado anaamka alfajiri kwenda kazini!

Why?

Jibu ni AMBITION. Na huwezi kuelewa.

Kwa sababu umeridhika na milioni mbili kwa mwezi. Unatukana watu Bar? Kisa unaendesha Subaru.

Ama umeridhika na milioni tatu kisa unatoa fungu la kumi laki 3 kwa mwezi. Hujui kuna watu fungu lao la kumi💰💰💰💰 ni kipato chako cha miaka 10 ijayo???

Mungu akiona unavyojidai moyoni anakucheka🤣🤣🤣

So why umeridhika my brother?
Kuna watu wameridhika kujenga nyumba moja. Kuna watu kwenda kusoma China au Marekani tu imewatosha. Huwaambii kitu.
Kuna watu kufanya kazi reception Vodacom tu karidhika. Hawazi kingine.
Kuna watu kupanga  chumba kimoja tu karidhika.
Wengine kumiliki TECNO tu imetosha 🤣🤣

Why umeridhika my sister?
Kuvaa high heels na kubarikiwa sura na mguu imetosha? Mke wa Mengi angeridhika na kuwa Miss Tanzania na kubweteka kama wengine angekuwa sijui wapi. Unajua kuolewa na Mengi akiwa anauza kalamu za wino kijijini haihitaji ambition sana. Lakini kuolewa na DR. REGINALD ABRAHAM MENGI tajiri, maarufu, millionaire anayetambulika duniani.. aisee hapo you've got to be ambitious.
Maana inahitaji UJIPANGE.
Mengi haoi MAKALIO. Anaoa MINDSET.
Sasa wewe umeridhika na Vitz na kupaka  lipstick akuoe wewe afu aamke alfajiri kujituma uanze kumwambia "Baby turidhike na tulichonacho baby"🤣

Kaolewe tu na mwenye Subaru kwa kweli mridhike vizuri kula chips mayai za mpemba huku mkiangalia series kwenye Star Times mpaka siku ya kufa.

Kuna watu kupata kazi Wizarani ndo kumeua AMBITION zao.
Kuna watu wameridhika kusaidia yatima mmoja na kumpost Instagram. Kuna watu kusomesha watoto wake ndo imetosha.
Unamtania Mungu.

Believe me. Uko hai ila hujui una deni kubwa mbele za Mungu. Na kuiona  makala  hii ujue una BAHATI. Serious. Kama unafikiri umeiona kwa bahati mbaya you don't know what you are reading.
Kuna watu wamekufa na wangetamani kusoma this article. 

Narudia...
Kama umebweteka umeridhika unajivutavuta kupiga hatua maishani Dangote anasema hupaswi kuwa hai.

And let me tell you now vizuri ili ujipime kuwa wewe pia unapaswa kuwa hai au la....

Listen to me very CLOSELY now!

Mungu wetu ni Mungu wa ambition.

Aliumba mtu mmoja akaona HAITOSHI.

Tumwekee msaidizi. Akampa Hawa.

Bado HAKURIDHIKA akawaambia sasa ZAENI MKAONGEZEKE.

BE FRUITFUL AND MULTIPLY.

That's AMBITION.

Mpaka leo hii Mungu hajasema sasa imetosha. No. Uumbaje kwake ni kitu very ambitious.

In other words kuwepo kwako duniani ni kwa sababu Mungu alikuwa hajaridhika na watu waliopo. Akakuleta na wewe uje kuongeza nguvu katika kuboresha dunia hii.

Umeboresha tayari?
Kama tayari basi muda wowote watu wanatype R.I.P.
Kama hujaboresha kitu hapa duniani na umeridhika hivyo hivyo wengine ndo wakuboreshee wewe ndo Dangote anasema hupaswi huwa hai. 

Hivi unajua AMBITION za wengine ndo zinakufanya upo Facebook leo na kuona makala hii na vitu vingine muhimu.

Facebook HAWAKURIDHIKA forum yao kuwa ya story tu kama Jamii Forums bali wameweka utaratibu wa kufanya biashara pia. Leo hii kuna vijana wanaingiza hadi milioni 6 kwa mwezi nchi hii kwa kuitumia Facebook kibiashara. Mwenye Facebook angekuwa karidhika tu watu kupiga story hapa asingekuwa pia tajiri namba 5 duniani kwa sasa.

Kutoridhika kwa watu fulani ndo kumekufanya wewe uwe na simu ya mkononi leo. Unapiga selfie siku nzima. Wangebweteka na simu za mezani ingekuwaje leo?

Kutoridhika kwa mtu kubaki na mawasiliano ya  barua za Posta tu ndo kumeleta Emails na instant messaging tools kama SMS, Messenger, WhatsApp, Viber, nk.

Kutoridhika kwa mzee Mengi ndo kumefanya watu zaidi ya 1500 wameajiriwa na makampuni yake leo hii. Uamuzi wa kutoka PWC na kwenda kuuza kalamu za wino ulimfikisha kwenye kuuza kiwi, hakuridhika akauza toilet paper, akauza detergents, dawa za meno, viatu, kufungua Gazeti la The Guardian mwaka 1994 na sasa ana magazeti takribani 11 watu wamesomea uandishi wa habari wanasongesha maisha. Because of him. 1995 akafungua ITV and leo Ana EATV na Capital TV. Na kuajiri watu wengi.
Halafu wao WAMERIDHIKA.

Waajiriwa wengi hawajui kuwa kutoridhika kwa bosi wao ndo kumesababisha wao waajiriwe. Wao wanaridhika. Hawataki kusababisha mwingine aajiriwe kama wao.

Huoni kuwa huo ni ubinafsi?

Ndo Dangote anasema kwa roho hiyo  hupaswi kuwa hai. Bado hujaelewa?

Fikiria Dongote.

Amezaliwa familia bora. Ya kitajiri. Angeweza kuridhika tu. But no. Aliamua kuomba mkopo aanzishe biashara yake pia.

Hakuridhika na biashara aliyoanza nayo. Sasa hivi anafanya biashara ya viwanda vya nguo, cement, benki, kilimo, petroli, sukari, chumvi, kampuni za simu, viwanda vya malori,.

Ameajiri  watu zaidi ya 30,000.

Thirty THOUSAND people directly employed!

Mtu mmoja tu huyo.

Halafu wewe ukiajiri dada wa kazi unaona umefanya maajabu kweli kweli.

Are you serious??

Halafu Dangote bado unasikia anataka kuwekeza kwenye soka.

Unajiuliza huyu haridhiki tu na hela?

Unadhani anatafuta hela.

No.

Hela alizonazo hawezi kuzimaliza.

Issue ni kusaidia watu wengi zaidi.

Ambition is for other people.

Kwa maana nyingine kama huna AMBITION it means you don't care about other people. Unajijali wewe tu. Sasa kwa nini upo hai bado? Watu wangejijali wao usingekuwa na hiyo simu nimekwambia.

Sikia.. Watu ambao hawaridhiki kirahisi ndo wanafanya wanaoridhika kirahisi wajione nao watu..

Kutoridhika kwa William Boeing ndo kumesababisha watu waone fahari kusafiri kwa ndege zake.
AMBITION.
Kutoridhika kwa Rais Magufuli ndo kulisababisha hiyo Boeing kuja Tanzania. Angeridhika na Bombardier hatua hiyo ya Boeing isingefikiwa. Kuna ajira zisingepatikana.

Kutoridhika kwa mtu mahali fulani ndo kumesababisha leo ukiingia  nyumbani kwako unabonyeza kitufe ukutani mwanga unatokea.
Anaitwa Thomas Edison.
Alijaribu mara 999 bila mafanikio.
Why?
Ambition!
Keshakufa long time. Lakini kaacha ALAMA isiyofutika.
Wewe utaacha nini? Subaru ya mkopo?

Kutoridhika kwa mtu mahali fulani ndo kumesababisha leo wewe unatuma pesa maelfu ya kilomita mbali na zinafika dakika hiyo hiyo na kutumika muda huo huo kadri ya uhitaji.

Hebu fikiria hao wote niliowataja kama wangeridhika tu na maisha. Hata hii makala usingeisoma.

Jifunze kwa hawa watu wawili.....

Nikiwa Kasulu Kigoma, nilifikia Highway Hotel... ndiyo hoteli maarufu zaidi Kasulu mjini. Nilipata fursa ya kukaa na mzee mwenye hiyo hoteli na kujifunza alikoanzia. Utashangaa mtu wa darasa  la nne ambaye leo ameajiri waliosoma zaidi yake na anasababisha waendeshe maisha yao. Kuanzia kwenye kuchuma chai Tanga na vibarua vya kuchimba visiki kujenga barabara. Hadi kumiliki hoteli na kuheshikima na mabenki na watu wakubwa serikalini. Yote hayo kwa sababu hakuridhika. Na hajaridhika. Anaendelea kuwekeza kwenye miradi mingine mingi. Utashangaa.

Think about that.

Then... Opposite na Highway Hotel upande wa pili wa barabara kuna vijana wadogo wanachoma kuku wa kienyeji kila jioni. Nikajenga urafiki na kijana mmoja wao hadi tukafikia level ya kuambiana mambo ya ndani ya kimaendeleo. Kaishia form two. Anachoma kuku kila jioni. Lakini sasa hivi anamiliki duka la simu ndogo za "tochi". Na anataka afikie kuuza smart phone. Anaita simu za "tachi". Na ndoto yake awe anafata simu hadi Dubai yeye mwenyewe!!! Na mke wake ndo hukaa dukani huko. Yeye anadeal na kuku. Na kila wiki faida ya kwenye kuku anaipeleka kwenye duka lake. Duka alifungua kwa mtaji wa milioni nne ikiwemo kodi milioni moja na laki mbili. Hela hiyo ilikusanywa kwa kuchoma kuku taratibu na kuweka faida. Biashara ya kuku alianza kwa laki moja. Laki moja aliipata kwa kufanya vibarua.

Unaposikia mtu huyo anakwambia kuhusu Dubai na yuko Kasulu anachoma kuku. Hajasoma kama wewe uliyefika chuo. Halafu wewe umeridhika. Yeye one day aje kuajiri watu 100 (akiwemo mwanao) wewe ukiwa Instagram unafatilia makalio ya Wema Sepetu.

Kwa nini uwe hai kweli?

Hivi unajua mtu kama Dangote hata Mungu akitaka kumchukua anasita kwanza. Maana mtu mmoja akitikisika uchumi wa nchi una-shake pia. Lakini kiukweli wengine nadhani Mungu wala hajiulizi. Anazima tu taa yako. Paap!
Watu wanatype R.I.P maisha yanaendelea.

Like seriously...

Mimi pia ningependa Mungu akitaka kunichukua kwanza anajiuliza maswali. Nikimchukua Andrea hili bara la Afrika kazi ya Andrea ataendeleza nani. Maana kazi nitakayomfanyia Mungu hapa duniani haina mfano wake. Nimeelewa kwa nini matajiri hawalali. Wanawaza wafanye nini ili wengine wapate ahueni ya maisha.

Strive Masiyiwa anabuni biashara kila kukicha. Sasa hivi yuko na KWESÉ SPORTS. Anaongeza ajira tu.
Kwa nini asiridhike tu na wakati yeye ndo tajiri namba moja Zimbabwe nzima?
AMBITION.

Dewji hatulii alisema ana ndoto ya kuajiri watu zaidi ya 20,000 Africa! Unadhani atawaajiri wapi? Means lazima abuni biashara mpya. Halali anawaza. Siyo ili apate  hela ya iPhone kama wewe. No anawaza ili wengine wapate ada, kodi, chakula, nk.

Bakhresa halali ameanzisha biashara nyingi tu na mpya nyingi now anaingia kwenye telecom.

Na mimi silali.

Nawaza how to help others wengi zaidi everyday. Sikutoka Stanbic sababu ya kutafuta hela ya kula au ya suti. No. Nilitoka ili kufanya vitu vikubwa ambavyo macho hayajapata kuona.

Sitalala.
Hata hii makala nayo nimeiandika kidogo kidogo jana huku nikitimiza majukumu mengine kutwa nzima. Lakini nikasema sitalala hadi niimalize. Niliimaliza saa nane na nusu usiku.

Why nisiridhike na makala ambazo nimeshaandika siku za nyuma?

AMBITION.

Kila siku nawaza niandike nini nichangie mawazo kwa wengine huenda yakawafaa na pamoja tukabadilisha maisha ya wengi. Najua niko hai kwa kazi maalumu. Ikiwemo hii.
And I'm doing it.
Sijui wewe.

Kama wewe umeridhika na ulipofikia it's fine.

Jay Z aliwahi kusema: "if you are okay being number two it's  alright but I'm not okay where you are."

But fikiria tu wote waliofanya vitu vikubwa wangeridhika na maisha yaliyokuwepo ingekuwaje.
Ungekuwa hapo ulipofika leo bila wengine kuwa na ambition?

Ukiamua kuridhika it's fine with me. BUT I'M NOT GOING TO SETTLE.

Good luck kwa wewe ambaye utaamua kupiga hatua mbele katika muda wako MCHACHE uliobakia hapa duniani.

Mungu wa mbinguni akutie nguvu.

Lakini kwa wewe ambaye umeridhika na ulipofika kasome tena title ya makala yangu.

Semper FEntrepreneur and Business Coach
Dar es Salaam, Tanzania
East Africa
WhatsA

No comments:

Post a Comment

KAZI KUU TANO (5) ZA IMANI KATIKA MAOMBI.

Bwana YESU atukuzwe ndugu zangu. Karibu tujifunze Neno la MUNGU. Uhusiano ni upendo unaozaa ushirikiano na mawasiliano kati ya pande m...