"Roho mtakatifu ni nani?"
Kuna utatanishi mwingi juu ya kumtambua Roho mtakatifu. Wengine
humchukulia kama nguvu Fulani zisizoonekana. Wengine huamini kwamba ni
uwezo wa Mungu ambao Mungu huuachilia maishani mwa wale ambao ni waumini
wa kristo. Je, biblia inasemaje juu ya Roho mtakatifu? Kwa kifupi
biblia inasema kwamba Roho mtakatifu ni Mungu. Pia biblia inasema kuwa
Roho mtakatifu ni mtu, mwenye akili, hisia na mapenzi yake.
Swala la kuwa Roho mtakatifu ni Mungu limo ndani ya aya nyingi za biblia
kama vile Matendo 5:3-4. Katika ayah ii petro anapambana na anania
aliyemdanganya Roho mtakatifu na nasisitiza yakuwa “hukumdanya mtu bali
Mungu.” Hili ni tangazo la wazi kwamba kumdanganya Roho mtakatifu ni
kumdanganya Mungu. Tunaweza pia kujua Roho mtakatifu ni Mungu kwa kuwa
ana tajwa na hali sawa na za Mungu. Roho mtakatifu yuko kila mahali
katika Zaburi 139:7-8, “nitaenda wapi nijifiche na Roho? ama
nitakimbilia wapi mbali na uwepo wako? Nikipanda juu mbinguni, huko uko;
nikifanya malazi yangu kuzimu, tazama uko huko,” tena katika wakorintho
wa Kwanza 2:10 tunaona hali yakuwepo kila mahali kwa Roho mtakatifu
“Lakini Mungu ameyajulisha kwetu kupitia Roho wake mtakatifu. Kwa kuwa
Roho huyachunguza mambo yote, naam, mambo ya siri ya Mungu. Kwa maana ni
nani ayajuaye ya mwanadamu isipokuwa roho ya mwanadamu inayokaa ndani
yake? Vivyo hivyo, hakuna ajuaye mambo ya Mungu isipokuwa Roho wa
Mungu.”
Tunaweza kujua kweli kwamba Roho mtakatifu ni Mungu kwa kuwa ana akili,
hisia na mapenzi yake. Roho mtakatifu hufikiri na hujua (Wakorintho wa
kwanza 2:10). Roho mtakatifu anaweza kuugua (Waefeso 4:30). Roho
hutuombea (Warumi 8:26-27). Roho mtakatifu hufanya maamuzi kutokana na
mapenzi yake mwenyewe (Wakorintho wa kwanza 12:7-11). Roho mtakatifu ni
Mungu, sehemu ya tatu ya utatu wa Mungu. Kama Mungu, Roho mtakatifu
anaweza kufanya kazi ya msaidizi na mshauri kama vile Yesu kristo
aliyevyoahidi kuwa atakuja kufanya (Yohana 14:16,26; 15:26).
Thursday, 23 November 2017
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
KAZI KUU TANO (5) ZA IMANI KATIKA MAOMBI.
Bwana YESU atukuzwe ndugu zangu. Karibu tujifunze Neno la MUNGU. Uhusiano ni upendo unaozaa ushirikiano na mawasiliano kati ya pande m...
-
Bwana YESU atukuzwe ndugu zangu. Karibu tujifunze Neno la MUNGU. Uhusiano ni upendo unaozaa ushirikiano na mawasiliano kati ya pande m...
-
Bwana Yesu asifiwe… Imeandikwa ; “ Bali wote waliompokea aliwapa uwezo wa kufanyika watoto wa Mungu, ndio wale waliaminio jina lake; “Y...
-
Ni miaka mingi nimekuwa nikijiuliza swali hili, nitawezaje kumpenda Mungu kwa moyo wangu wote, kwa akili zangu zote na kwa nguvu zangu zote...
No comments:
Post a Comment