Bwana Yesu asifiwe…
Kwa ufupi…
02. Kiburi cha uzima.
Kiburi ni mojawapo ya sababu kubwa
inayowafanya wengi kushindwa kuishi maisha ya utii. Kiburi cha uzima ni
hali ya kutomuhitaji Mungu kwa sababu una utele fulani hivi, kwamba wewe
ni mzima, mambo yako unaona yanaenda vizuri hivi, sasa unajikuta
ukishindwa kufanya mapenzi ya Mungu.
Mtu mwenye kiburi cha uzima, kamwe hawezi kutembea na Mungu wake katika utii. Kwa sababu anajiuliza maswali mengi, kama vile “kuna haja gani ya kuomba wakati nina kila kitu ndani?” Mfano
; mchungaji wake akimwambia afunge na kuomba,utakuta hawezi kwa sababu
ya kiburi cha uzima alichonacho. Sijui kama unanielewa?
Si watu wote wenye mali hawana utii,wala
si watu wote walio na afya njema wamekosa utii,bali wengi wa wenye mali
hawana utii wa neno la Mungu ipasavyo na ndio maana hata Yesu alisema
kwamba ni shida tajiri kuingia katika ufalme wa mbinguni ( Mathayo
19:23). Na si tajiri tu bali wengi wetu wenye afya nzuri tunasumbuliwa
na kiburi cha uzima,kwa hiyo maagizo ya Bwana hatuyatilii mkazo kwa
sababu tu wazima leo, lakini tumesahau kwamba ikiwa leo tu wazima kesho
tunaweza kuwa wagonjwa.!
Wewe je,upoje katika eneo hili? Je ni
kweli inajitahidi kutimiza mapenzi ya Mungu au unaacha kwa sababu upo na
uzima sasa. Ni mara ngapi unakaidi sauti ya Mungu kwa kinywa cha
mchungaji wako pale akuambiapo neno la Mungu? Kisha usifanye sawasawa na
badala yake ukafanya mambo yako?
Nimeona wengi wakitembea nje ya utii wa
sauti ya Mungu kwa kinywa cha wachungaji wao. Wengine husema sina muda
sasa kufanya hivyo mchungaji atakavyo,lakini papo hapo ana muda wa
kufanya mambo yake tena wakati mwingine hayo mambo yake ni mambo
machafu!!! Ikiwa ni hivi basi mtu wa namna hii amekosa utii wa kawaida
kabisa. Na kundi la namna hii lipo kubwa sana makanisani mwetu, lakini
ni kwa sababu ya kuwa na kiburi cha uzima.
Biblia inakutaka usije ukamsahau Bwana
Mungu wako pindi utakapofanikiwa kwa namna yoyote ile ( Kumbukumbu
8:11-17). Ukiwa katika afya uliyonayo hapo ndipo ujitoe zaidi kwa Bwana
Mungu katika kuhakikisha unafanya yote akuagizayo Bwana Mungu wako.
Kumbuka Mungu huwapinga wenye kiburi (1
Petro 5:5). Hii ikiwa na maana wenye kiburi wamekosa nafasi kwa Mungu
wamekataliwa. Kwa sababu kiburi chochote kile ni tabia ya shetani.
Ibilisi hali akijua kwamba ili ushindwe kuwa pamoja na Mungu basi
amepanda kiburi kama roho ndani yako kwa kusudi wewe umekosea Mungu
ushindwe kuwa mtii.
Kiburi cha uzima ni hatari sana;
Siku moja nilikuwa
nikiongea na mmoja wa mtoto wangu wa kiroho aliyekuwa akiishi nje ya
nchi. Ulikuwa akiishi ulaya huko katikati ya wazungu ingawa yeye ni
mtanzania mwenzangu. Sasa ananiambia kwamba mahali alipo hakuna kabisa
mambo ya ibada za kiroho kama hizi tuzifanyazo huku kwetu Tanzania maana
yeye alikuwa ameokoka. Alitegemea kuwakuta wazungu wa mahali pale alipo
kwamba ni watu ambao watakuwa na hofu na Mungu,wakiwa ni wapendwa
waliookoka; lakini hakukuta hivyo
Bali alikuta kila mzungu
ana maisha yake kivyake vyake wala hakuna mambo ya ibada za kiroho. Kwa
maana hao watu waliomzunguka hawakuona sababu ya kuomba omba kwa Mungu
maana wana kila kitu ndani. Wana magari,pesa.! Hivyo hata wengine
hawaamini wokovu. Ndio, wanaamini kuwa Mungu yupo lakini so what ! Kama
yupo.
Hivyo hana haja hata ya
kwenda kanisani. Ananiambia kwamba wale wenye kuenda kanisani ni wazee
fulani hivi tena ni wachache tu tena hakuna kanisa la kiroho bali yapo
tu kanisa la kawaida kabisa wanafanya ibada kifamilia hivi kisha
wanaondoka zao.
Sasa,kinachowasumbua hawa
watu ni kiburi cha uzima kama moja ya sababu ya kuwafanya watu hao
wasifanye mapenzi ya Mungu kwa dhati maana wanajiona wamekamilika.
Lakini mimi nataka nikuambie,hatutembei kwenye utii kwa sababu
tunahitaji kuwa na majumba au magari au mali fulani! Bali tunayafanya
mapenzi ya Mungu kwa sababu ya kukamilishwa katika wokovu wetu maana
utii ni njia ya wokovu kamili.
Mpendwa,ebu jichunguze
uone kana kwamba una tabia hii ya kiburi cha uzima kwa sababu ya
afya,mali,ulizonazo. Kumbuka kwamba afya,pesa,mali zote ni za Bwana
Mungu. Yeye Mungu amekuaminisha tu,wala si za kwako maana akitaka
kuzichukua anaweza kuzichukua saa yoyote ile na hakuna mahali pale
kushtaki!
Ile namna ya kuwa na
kiburi ni pandikizi la shetani ndani yako. Ile namna ya kujiona wewe ni
bora zaidi ya wengine kunakufanya usimfuate Mungu ipasavyo. Kwa nini
unapuuzia sauti ya Mungu? Mfano; umehubiriwa vya kutosha kuhusu wokovu
lakini unakataa na kuona kwamba kuokoka ni mambo ya hao wasio na kazi
maalumu,au unaona masuala ya Mungu ni ya watu maskini hivi! Wewe kwamba
huna muda huo wa kukaa na watu wasio na elimu,watu wachovu wachovu hivi!
Ukiwa na mawazo ya namna hiyo basi ni kiburi cha uzima ndicho
kinachokusumbua
Lengo kuu la ujumbe huu
ni kukufanya sasa ushuke na unyenyekee kwa Bwana ukihakikisha unayafanya
mapenzi ya Mungu kwa bidii na huko ndiko kutembea na Mungu katika utii
ninakokuzungumzia.
Kilichowafanya akina Adamu kuanguka ni wazo la kiburi kutoka kwa ibilisi nyoka aliwaambia “mkila matunda ya mti wa ujuzi wa mema na mabaya, mtafumbuliwa macho na kuwa kama Mungu” akina
Adamu wakatamani kuwa kama Mungu hali wao ni wanadamu ikiwa wanafanana
sana na Mungu. Kule kutaka kuwa kama Mungu alivyo ni kiburi ndani yao.
Sasa,ikiwa unahisi hali fulani ya kushindwa kutembea katika njia ya utii kwa sababu kuna hali fulani ya kiburi,(au hali yoyote ile) basi nipigie simu yangu hizi;
No comments:
Post a Comment