• Mwanzo 28: 10-15 Yakobo alipokuwa anamkimbia ndugu yake Esau anakutana na
malango ya mbinguni mahali alipolala aliona ngazi na Malaika wanapanda na kushuka.
• Madhabahu inafungua malango ya Mbinguni.
Unapomjengea Mungu Madhabahu katika maisha yako unafungua malango ya Mbinguni kwa kuweza wewe kuwasiliana na Mungu.
• Shetani naye huiga vitu vya Mungu.
Unapokuwa na madhabahu ya shetani, na yenyewe ina malango yake na yeye kuweza kukutumia ipasavyo.
• Babu zetu walikwenda kwa shetani kufanya agano naye.
Isaya 28:15 Tunafanya agano na mauti na kupatana na kuzimu.
• Unapoenda kwenye Madhabahu ya shetani kuna karama zake: Ulevi, wizi, uasherati na uzinzi, uchawi, uongo, masengenyo n.k.
• Shetani ameiga vitu vingi vya Mungu.
Mungu alimwambia Ibrahimu amtoe mtoto wake sadaka na shetani anawaambia watu watoe watoto sadaka.
• Fanya utafiti katika maisha yako ni mambo gani magumu ambayo yameshika maisha yako.
• Fanya utafiti katika maisha yako na familia yako walikuwa wanafanya mambo gani katika ukoo wenu.
• Kuna mambo magumu katika ukoo wenu ambayo hayafunguki
• Mfano: Kutokuolewa au kuoa, kutokufanikiwa, magonjwa n.k.
Kutoka 20: 1-6
2Falme 17:17
• Ni muhimu kuingia katika toba na kufunga na kuomba. Muulize Mungu katika mambo yaliyo magumu.
• Toba ndiyo mlango wa kutokea,
• Anza na toba, Toba inafungua malango.
No comments:
Post a Comment