• Kumb 18: 10-12,
Kumb 13: 6-8
2 Falme 17: 17
• Katika Madhabahu hizo watu wanakuja na kuwasiliana na roho ya shetani
Isaya 28: 15
Maombolezo 5: 7
• Katika Madhabahu hizo kuna maagano yanafanyika na watu wanaotoa kafara wanatoa watu, watoto, wanyama, mazao n.k.
Isaya 26: 21
Hesabu 35: 33
• Shetani amewadanganya babu zetu katika mila na desturi zetu katika kila madhabahu kunakuwa na makuhani wanaohudumia mahali pale.
Kumb 13: 6-8
Kumb 18: 10-12
Walawi 20: 27
• Kuhani husimama kati ya watu na Mungu, sisi ni makuhani wa kifalme.
• Sisi kama watu tuliochaguliwa kama makuhani na tuyafanye yale ambayo tunatakiwa tuyatamke,
Isaya 8: 10
Yeremia 22: 29-30 unapoona mambo hayaendi sawasawa na Mpango wa Mungu hakuna haki inayotendeka, hata katika serikali n.k. Tamka neon maneno yako yana nguvu.
Isaya 49: 1-2
Mathayo 18: 18 Lolote mtakalolifunga duniani na mbinguni litafungwa
3. MAKUSUDI YA MUNGU YA KUWA NA MADHABAHU
• Zaburi 115; 16 -17
• Mwanzo 1 : 26 – Dunia ilijengwa kwa sababu ya wanadamu ili waweze kumsifu Mungu
na kumwabudu.
• Mwanzo 12: 1 -9 – Maisha ya Abrahamu yalikuwa ya kutembea kabla hajamiliki nchi aliyopewa. Abrahamu alitengeneza madhahabu ya kwanza madhahabu ya eneo
• Madhahabu za kifamilia na za kikabila hizo madhahabu zina nguvu katika familia.Kuwa mwangalifu kwa mambo ya mila tunzojiingiza
• Mwanzo 13:14-18 unapotembea katika mji na kutoa (Unabii) maneno ya kinabii, maneno haya yanakuwa na nguvu sana.
Mwanzo 15:8-9/ 18-21
Mungu anathibitisha tena juu ya ahadi yake, juu ya Ibrahimu.
• Ibrahimu anamwambia Mungu nitajuaje kuwa utanipa lini hii nchi? Mungu anamwambia nijengee madhabahu.
• Mwanzo 26: 23-25 Isaka pia alijenga madhabahu ya Mungu.
• Mwanzo 28:11- 15, 21 Yakobo ni Mjukuu wa Ibrahimu wakati anamkimbia kaka yake Esau baada ya kumuibia uzaliwa wake wa kwanza.
• Analala eneo ambalo babu yake Ibrhimu alimjengea Mungu madhabahu
Mstari 16 Yakobo akasema kweli Mungu yupo mahali hapa.
Mstari 12 Malaika walikuwa wanapanda juu na kushuka ina maana Malaika walikuwa hapo chini wakilinda.
• Mwanzo 32: 1-2 Yakobo tena anakutana na malaika alipokuwa anarudi, eneo hilo ni maeneo ambayo babu yake ibrahimu alikuwa anamjengea Mungu madhabahu.
• Unapomjengea Mungu madhabahu panakuwa ni malango ya mbinguni.
Mathayo 16: 18 nitalijenga kanisa langu na malango ya kuzimu hayatalishinda.
• Ni muhimu sana kwa kanisa kujua malango ya kuzimu.
• Kuna madhabahu inayovuta giza. Ni vigumu maeneo mengine watu (kuokoka) kupokea wokovu kwa sababu ya madhabahu zilizopo.
• Watu wengine wanatumia madhabahu kuweka ulinzi katika maeneo wanayoishi.
Kutoa sadaka kabla hawajajenga nyumba
• Sisi ni makuhani wa Bwana ni lazima tuchukue hatua kukataa nguvu za madhabahu nyingine.
• Kumb 28: 43 Mgeni atakua na nguvu kuliko wewe mwenyeji leo hii tunaona wageni ndio wenye nguvu katika nchi yetu wanatutawala.
• Mwanzo 33;18-20 Yakobo alinunua nchi. Mstari 20 akamjengea Mungu Madhabahu.
• Unaponunua ardhi usivamie tu na kujenga vunja kwanza madhabahu ya Shetani na umjengee Mungu Madhabahu.
• Mwanzo 35:11-14 Yakobo akasimamisha nguzo mahali aliposema na Mungu, nguzo ya mawe akaimimina sadaka ya kinywaji na mafuta juu yake.
• Maeneo mengi ya milima huwa shetani anayatumia kwa Madhabahu yake.
Zaburi 24:1 Nchi na vyote viijazavyo ni mali ya Bwana Vilima na vyote ni mali ya Bwana.
• Inawezekana Madhabahu nyingine ipo ndani ya mwili wako.
• Mfano: kuchanja chale hizo ni Madhabahu za shetani inabidi kuzishughulikia.
Walawi 19:28
• Juu ya kutofanikiwa katika maisha au familia yako.
Chukua hatua muulize Mungu.
• Pia kuna Madhabahu ya kitaifa. Hii inafanya kazi sana, na hii hatuwezi kuishughulikia mpaka tuwe katika umoja.
No comments:
Post a Comment