IMANI YAKO IKO WAPI? – NA MCH.KIRIMBAI
*Petro akamjibu, akasema, Bwana, ikiwa ni wewe, niamuru nije kwako juu ya maji. Akasema, Njoo. Petro akashuka katika mashua, akatembea juu ya maji, ili kumwendea Yesu. Lakini alipouona upepo, akaogopa; akaanza kuzama, akapiga yowe, akisema, Bwana, niokoe. Mara Yesu akanyosha mkono wake, akamshika, akamwambia, Ewe mwenye imani haba, mbona uliona shaka? (Mathayo 14:28-31 SUV).*
Petro na wenzie walikuwa wanavuka ziwa kwenda upande wa pili walipokutana na bonge la dhoruba njiani.
Hali ilikuwa mbaya mno na walikuwa hatarini kupoteza chombo chao na uhai wao alafu ghafla katika ile ile hali ya bahari kuchafuka na dhoruba wanamwona Yesu anakuja akitembea juu ya maji.
Kwa kuwa halikuwa jambo la kawaida wanafunzi wakaogopa mno wakidhani ni mzimu ila Yesu akawadhibitishia ni Yeye.
Petro bado hakuwa na uhakika akamwambia Yesu kama kweli ni wewe niamuru nije juu ya maji.
Yesu akaachilia tu Neno moja na kumwambia njoo.
Petro akashuka toka chomboni huku bahari ikiwa imechafuka vile vile akatembea juu ya maji.
Sio kila wakati Yesu atatuliza dhoruba iliyopo maishani mwako lakini uwe na uhakika atakupa Neno litakalo kuwezesha kusonga mbele pamoja na dhoruba inayoendelea.
Petro aliliamini Neno alilopewa na Yesu akatembea juu ya maji na dhoruba ikiwa inaendelea.
Hata wewe unaweza ukaliamini Neno la Yesu na ukaendelea na maisha pamoja na changamoto zilizopo.
Kosa alilofanya Petro ni kutazama kilichokuwa kinaendelea kumzunguka akaacha kumwangalia Yesu na Neno aliloachilia kwake akaanza kuzama.
Ukiondoa macho yako kwa Yesu na kwa Neno alilokupa changamoto zilizokuzunguka zitaanza kukumeza.
Lakini Petro akapaza sauti yake akasema Bwana niokoe.
Hata wewe kwenye hali yako ya kuzama na kumezwa na changamoto yako unaweza kupaza sauti yako na kuliitia Jina la Bwana maana kila atakayeliitia Jina la Bwana ataokolewa.
Nawe utakapoliitia Jina la Bwana kama Petro utaokolewa.
Kwanini uwaze na kuumia wakati Yesu yupo.
Yu hai leo.
Mwiite Naye atakuitika atakuonyesha mambo makubwa magumu usiyoyajua.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
KAZI KUU TANO (5) ZA IMANI KATIKA MAOMBI.
Bwana YESU atukuzwe ndugu zangu. Karibu tujifunze Neno la MUNGU. Uhusiano ni upendo unaozaa ushirikiano na mawasiliano kati ya pande m...
-
Bwana YESU atukuzwe ndugu zangu. Karibu tujifunze Neno la MUNGU. Uhusiano ni upendo unaozaa ushirikiano na mawasiliano kati ya pande m...
-
Bwana Yesu asifiwe… Imeandikwa ; “ Bali wote waliompokea aliwapa uwezo wa kufanyika watoto wa Mungu, ndio wale waliaminio jina lake; “Y...
-
Ni miaka mingi nimekuwa nikijiuliza swali hili, nitawezaje kumpenda Mungu kwa moyo wangu wote, kwa akili zangu zote na kwa nguvu zangu zote...
No comments:
Post a Comment