Ebu fikiria Dada anayechoma mahindi maeneo ya Manzese Darajani kuanzia saa 12 jioni mpaka SAA 2 usiku, kwa siku moja anauwezo wa kuchoma mahindi .50. Kila hindi moja ananunua shambani kwa shilingi 100/- Na Anauza kwa sh.600/-
Hiyo ina maana mahindi 50 ananunua kwa shilingi 5000/- akichoma na kuuza anapata sh.30,000/-. Akitoa pesa ya mtaji (5000/- ya mahindi na 1500/- ya mkaa) anabakiwa na sh.23,500/- kwa siku.
Hivyo kwa mwezi huyu mchoma mahindi atakuwa ameingiza kiasi cha sh.705,000/-
Mwalimu mwenye Degree anayeanza kazi analipwa 584,000/- akikatwa kodi pamoja na makato mengene ya mifuko ya jamii anabakiwa na sh.425,000/.
Tofauti ya Mwalimu wa degree na Muuza mahindi ni
Kuwa Mwalimu kanaajiriwa,
muuza mahindi kajiajiri.
Mwalimu anafanya kazi masaa 9 kwa siku (saa2 asubuh hadi 11jioni)
muuza mahindi anafanya kazi masaa matatu kwa siku (saa 12 jioni hadi 2 usiku).
Mwalimu anatumia muda wake wa ziada kusahihisha mitihani na homework,
mchoma mahindi anatumia muda wake wa ziada kutafuta fursa nyingine za kupata hela zaidi..
UOGA WAKO NDIO UMASKINI WAKO..
No comments:
Post a Comment