Ni jambo la muhimu sana mzazi ukiwa na utaratibu wa kuwaombea watoto wako katika maisha yao na kila jambo linalohusiana nao.
1. Waombee wamjue Mungu tangu wakiwa na umri mdogo.
2Timotheo 3:15 na jinsi ambavyo tangu utoto wako umeyafahamu Maandiko matakatifu ambayo yanaweza kukuelekeza kupokea wokovu kwa kumwamini Kristo Yesu.
2. Waombee waichukie dhambi
Zaburi 97:10 Wale wanaompenda BWANA na wauchukie uovu,
kwa maana Yeye hulinda maisha ya waaminifu wake
na kuwaokoa kutoka mkononi mwa mwovu
3. Wawe salama na kupata ulinzi mbali na mwovu katika maisha yao ya kiroho, kimwili na kihisia.
Yohana 17:15 Siombi kwamba uwaondoe ulimwenguni, bali uwalinde na yule mwovu shetani
4. Wawe watu wema katika mahusiano yao na watu wengine.
Daniel 6:3 Basi Danieli alijidhihirisha mwenyewe, miongoni mwa wasimamizi na maliwali kwa sifa zake za kipekee hata mfalme akapanga kumweka juu ya ufalme wote.
5. Wakue wakiheshimu mamlaka zilizo juu yao
Warumi 13:1 Kila mtu hana budi kutii serikali inayotawala. Kwa maana hakuna mamlaka isiyotoka kwa Mungu; na serikali zote zilizopo zimewekwa na Mungu
6. Wawe na marafiki wema na waweze kuepuka marafiki wabaya.
Mithali 1:10 Mwanangu, kama wenye dhambi
wakikushawishi,usikubaliane nao
7. Wakue na kupata wenzi wema toka kwa Bwana na kuepushwa na wenzi wasiofaa.
2Kor 6:14 Msifungiwe nira pamoja na wasioamini. Kwa maana kuna uhusiano gani kati ya haki na uovu? Au kuna ushirika gani kati ya nuru na giza
8. Waweze kujifunza na kujitoa kwa Mungu kikamilifu na kuweza kumpinga shetani
Yakobo 4:7-8 Kwa hiyo, jinyenyekezeni kwa Mungu . Mpingeni shetani, naye atawakimbia. 8Mkaribieni Mungu, naye atawakaribia. Takaseni mikono yenu, ninyi wenye dhambi; na takaseni mioyo yenu, ninyi wenye nia mbili
Mungu atusaidie sana.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
KAZI KUU TANO (5) ZA IMANI KATIKA MAOMBI.
Bwana YESU atukuzwe ndugu zangu. Karibu tujifunze Neno la MUNGU. Uhusiano ni upendo unaozaa ushirikiano na mawasiliano kati ya pande m...
-
Bwana YESU atukuzwe ndugu zangu. Karibu tujifunze Neno la MUNGU. Uhusiano ni upendo unaozaa ushirikiano na mawasiliano kati ya pande m...
-
Bwana Yesu asifiwe… Imeandikwa ; “ Bali wote waliompokea aliwapa uwezo wa kufanyika watoto wa Mungu, ndio wale waliaminio jina lake; “Y...
-
Ni miaka mingi nimekuwa nikijiuliza swali hili, nitawezaje kumpenda Mungu kwa moyo wangu wote, kwa akili zangu zote na kwa nguvu zangu zote...

No comments:
Post a Comment