Thursday, 11 October 2018

Aina nyingine za sadaka

 Aina nyingine za sadaka

 Image result for aina za sadaka kibiblia
 3.  FUNGU LA KUMI na ZAKA: Hizi ni sadaka ambazo ni lazima kutoa tena kwa ukamilifu. Malaki 3:7-10…” Pia soma Matendo 5:1-10 …utaona habari za ANANIA na SAFIRA mkewe ambao wote walikufa mbele ya mitume (petro) kwa kosa la kutokutoa walicho ahidi kwa ukamilifu na kujaribu kuficha sahemu ahadi yao kwa siri..
NANI ANAPASWA KUTOA FUNGU LA KUMI?
Kimsingi na katika mfumo wa Neno au Biblia Takatifu mtu anayepaswa kutoa sadaka hii ni yule aliyepewa riziki na Mwenyezi Mungu,mtu aliyewezeshwa au kufanikishwa,kurithishwa au kupewa mali ya kutumia/matumizi kaatiaka maisha ya kila siku.
Kwa mfano huu twajifunza: Mtu mmoja alilima shamba na mazao ya shamba yakastawi kwa ukubwa( hata kwa uchache) akalima nyasi zikatoka, mimea ikazaa mbegu na kiangazi kikalifikia shamba,mwenye shamba akapeleka vibarua wakafanya kazi shambani mwake wakivuna wingi wa  magunia/mifuko ipatayo mia moja (100). Katika mazao hayo kwa unyoofu na uaminifu mtu huyo kabla ya kuyatumia au kutoa hesabu yoyote akaitoa sehemu ya kumi ya mifuko hiyo na kupeleka mezani kwa Bwana. akalitimiza agano akabarikiwa!! Hivyo sasa kumbe mtu anayepaswa kutoa fungu la kumi ni Yule aliyetafuta,kutunza alichopewa,kukiendeleza. au chanzo cha mapato yaliyohalali kwa mtu yeyote yule ambaye ni mwamini( aliyeokoka). 
 NI WAKATI UPI WA KUTOA FUNGU LA KUMI?
Imezoeleka sana kwa waamini kwamba wakati wa kutoa fungu la kumi ni pale anapoona yeye inafaa hata kama anavyo kwaajili ya Bwana lakini yeye atasubiri amani ya moyo iamue(wakati mwingine tunaiita ni roho ya kumfundisha Mungu jinsi ya kutoa), huu ni wizi mkubwa! Pia watu wanasema wakati wa kutoa au siku ya kutoa ni siku ya kuabudu kama vile jumapili, na ibada za katikati kama jumanne,ijumaa na  jumatano kitu ambacho ni kumdanganya Mungu. Kwani wakati wa kumpelekea Mungu kilicho kitakatifu chake ni siku/ wakati wowote ule maadamu kimepatikana kutoka katika mikono yako iliyopewa mamlaka nayeye aliyekupa na kuvifanya kwa ajili yako.( hakuna siku maalumu ya kumtolea Bwana fungu la kumi bali ni wakati na siku yoyote Bwana akileta yakupasa nawe upeleke kwake sehemu ya kumi kama agano au mkataba kati ya mwamini na Mungu).Kumbuka pia milango ya hekalu haifungwi kwa maana ya kiroho.
 Kabla ya kumtolea Bwana sehemu ya kumi ni lazima tujitakase na kutafakari uharali wa kipato au mali ulipochota sehemu hiyo ya  kumi. Mungu anachukizwa na vitu vilema yaani sadaka kilema au yenye kasoro. Kwa mfano mtu aliyeiba hafai kupeleka sehemu ya kumi kwa Mungu kwa mali alizoiba kwa jirani yake. Pia mtu aliyetenda dhambi(kama vile uzinzi,uasherati,usengenyaji,uoga n.k) hafai mbele za Bwana hata kama ameipeleka sehemu hiyo ya kumi kwa uchache au kwa wingi kiasi gani bali kinacho angaliwa ni uhusiano wa  mali na mtu na Mungu anayekwenda kuvipokea na kuvitakasa kwa ajili ya meza/ nyumba yake. Hivyo  twasema mtua aliyetenda dhambi hapaswi kupeleka sadaka hiyo mbele za Mungu kwani ni chukizo wala sadaka hiyo haitamfikia Mungu patakatifu pake ( itatupiliwa mbali kabla haijafika). Tukisoms katika kitabu kitakatifu cha Mithali ya 15:8 neno linasema hivi; “Sadaka ya mtu mbaya ni chukizo  kwa Bwana; bali maombi ya mtu mnyofu ni furaha yake”.Hivyo sadaka iliyoambatana na uchafu haifai mbele za Bwana aliyetukuka.
Mwamini aliyetenda dhambi naajitakase kisha akamtolee Bwana sehemu ya kumi, bila kujitakasa huyo afanya bure wala hawezi kupokea majibu ya sadaka yake katika sehemu yoyote ya kipato kama vile shambani, ofisini,mifugo na biashara.MUNGU ANAJIBU.
 FUNGU LA KUMI LINATOLEWA WAPI?  
Fungu la kumi linatolewa kanisani/hekaluni pa kuabudia au nyumbani mwa Bwana na hayupo mwingine wa kulipokea hilo fungu la kumi isipokuwa Mungu aliyeagiza. Pia fungu la kumi ikumbukwe halitolewi sokoni,shuleni au katika makongamano ya injili bali ni kanisani tu! Kwenda kinyume na haya ni kumwibia Mungu na ni dhambi kuiba dhabihu na zaka ya Bwana. Malaki 3:8-9 “Je! Mwanadamu atamwibia mungu? Lakini ninyi mnaniibia mimi. Lakini ninyi mwasema, tumekuibia  kwa namna gani? Mmeniibia zaka na dhabihu. Ninyi mmelaaniwa kwa laana; maana mnaniibia mimi,naam taifa hili lote. Leteni zaka kamili ghalani,ili kiwemo chakula katika nyumba yangu…”. Hivyo twajua sasa kwamba sehemu ya kumi itapelekwa  kanisani  na si mahali pengine. MUNGU ANAJIBU.
KWANINI TUNATOA FUNGU LA KUMI?
Hili pia ni swali ambalo limekuwa mbele san kwa waaminni kujiuliza juu ya kutoa kwa fungu la kumi.
Wapendwa kikubwa cha kujifunza hapa ni kwamba lazima tujue ni nani aliweka au kututaka tutoe fungu la kumi, na kwanini alitutaka, pia kunafaida gani ya kulifuata agano hili. Hapa yote yameelezwa hapo juu lakini sasa tutaona kwa nini tunatoa fungu la kumi? .
Tunatoa fungu la kumi ili kuipendezesha nyumba ya mungu au kufanya utajiri nyumba ya Bwana wakati wote na kuifanya kutokuwa na ukiwa au kupunguka kwa hali zote. Nyumba ya Bwana hujazwa na watakatifu wake waliolishika agano lake  na kunyenyekea mbele zake. Tunasoma kitabu cha  Yohana Mtakatifu  4:34 ambapo Neno linasema;
 “Akawaambia ,mimi ninacho chakula msichokijua ninyi, basi wanafunzi wake wakasemezana, Je! mtu amemletea chakula? Yesu akawaambia, chakula change ndicho hiki, niyatende mapenzi yake aliyenipeleka nikaimalize kazi yake”. Lakini mfano huu hautoshi kwako bali kaa katika Neno na kutafakari juu ya sadaka ya sehemu ya kumi.
FAIDA ZA KUTOA SEHEMU YA KUMI
Fungu la kumi huondoa mikosi. Mtu aliyeokoka anaweza kuendelea kuwa mshindi kwa kuyashinda maagano siku hadi siku kwa kuwapiga maadui kwa fimbo ya fungu la kumi lililoambatana na utakatifu. kwa mfano baadhi ya familia zinatoka katika koo ambazo zinajivunia magonjwa ya kuruthi na tabia mbaya za kurithi kama vile watoto kuzaliwa walemavu,umasikini na tabia nyingine kama vile za wizi, uasherati na uzinzi ambazo kwa namna moja au nyingine nazo ni pepo. Kupitia fungu la kumi mtu huyashinda haya yote kwani Bwana wa vita atasambaratisha tabia zote ambazo ni tabia tata na kupanda mbegu za mizabibu inayozaa na familia au koo hiyo itabarikiwa na kuitwa Heri mbele ya mataifa yote. Kwa mfano mzuri tunasoma kitabu cha Malaki 3:12 “Na mataifa yote  watawaiteni heri; maana mtakuwa nchi ya kupendeza sana , asema Bwana wa majeshi”. Hapa hapana mpinzani kwani wengi tumashahidi katika hili kwa wote waliowaaminifu katika sehemu ya kumi huitwa heri (The Blessed). MUNGU ANAJIBU.
Fungu la kumi huruhusu mafanikio kwa kuziruhusu Baraka kumfikia mtoaji wa sehemu ya kumi. Kwa uaminifu mkubwa Mungu huyaachiria madirisha yake kumuelekea mwanadamu aliye mwaminifu katika kumtolea sehemu hiyo ya kumi, yaani huruhusu Baraka kumfuata yule aliyemwaminifu kwa sehemu ya kumi. Twasoma Malaki 3:10 “ Leteni zaka kamili ghalani, ili kiwemo chakula katika nyumba yangu,mkanijaribu kwa njia hiyo, asema Bwana wa majeshi; mjue kama sitawafungulia madirisha ya mbinguni,na kuwamwagieni baraka,hata isiwepo nafasi ya kutosha au la.” Kumbe sasa twajua ya kwamba kupitia fungu la kumi tunaweza kuyafanya madirisha ya mbinguni kufunguka Na baraka kutuelekea sisi tuliowake na waaminifu katika sehemu ya kumi (fungu la kumi).MUNGU ANAJIBU.
Fungu la kumi ni ulinzi katika mambo yote ya mtu aliyeamini na mtoaji wa sehemu hiyo. Hapa tunajifunza kuwaMungu Baba wa Yesu Kristo ni Bwana wa majeshi na ni mtoaji wa majeshi ya kulinda mipaka ya wale walio katika arabuni yake. Kupitia sehemu ya kumi kama sadaka ya agano kati ya Mungu na mwamini tunawashinda maadui zetu na kuwaacha mbali sana kwani Mungu tunayemtolea nia Mungu wa viwango. Mungu huleta ulinzi Kwa kila tunachokifanya ambacho kinampendeza. Malaki 3:11 “Nami kwa ajili yenu nitamkemea yeye alaye,wala hataharibu mazao ya ardhi yenu; wala mzabibu wenu hautapukutisha matunda yake kabla ya wakati wake katika mashamba,asema Bwana wa majeshi.” Kumbe Bwana wa majeshi atayatuma majeshi yake kulinda na kushambulia majeshi dhaifu ya shetani na hawatatuweza kwa njia hii ya kumtolea Bwana kilicho kitakatifu chake wakati wote ( sehemu ya kumi).
 4.  Malimbuko: Hii ni sadaka ya mzaliwa wa kwanza. (a) Mshahara wako wa kwanza (kama mzaliwa wa kwanza) wote- sadaka kwa Mungu (b) Faida ya mapato ya kwanza-biashara, kilimo.. Mithali 3:9-10 .. .”…mheshimu Bwana kwa mali yako, na kwa malimbuko ya mazao yako yote. ndipo ghala zako zitakapojazwa kwa wingi….Pia soma Nehemia 12:44 , kumbukumbu 26:1-2 , 2nyakati 31:4-6 
5. Dhabihu : Hii ni sadaka ambayo roho mtakatifu husema na wewe moja kwa moja.. mwanzo 22:1-3… utaona habari za Ibrahimu

6. SADAKA YA AMANII
Sadaka ya namna hii hutolewa kwa lengo kuu la kutamka amani katika maeneo mbalimbali ambapo mwanadamu aliyeamini katika Kristo kuruhusu amani itawale katika maeneo hayo. hili ni suala la kiroho pia kwani limeonekana katika Biblia takatifu pale kitabu cha Kutoka 32:6 “wakaondka asubuhi na mapema,wakatoa dhabihu, wakaleta sadaka za amani,watu wakaketi kula na kunywa,wakaondoka wacheze”. Hivyo sadaka hii huleta amani katika maeneo mbalimbali ikiwemo ndani ya familia (ndoa), taifa na maofisini.MUNGU ANAJIBU.

7. SADAKA YA KUINULIWA
Katika Kitabu cha Kumbukumbu la Torati 12:11 “Wakati huo itakuwa kwambamahali pale atakapo pachagua Bwana,Mungu wenu, alikalishe jina lake ,hapo ndipo mtakapoleta  kila kitu ninachowaamuru,sadaka zenu za kuteketezwa…na sadaka ya kuinuliwa ya mikono yenu…”. Sadaka hii ni ile ambayo kwa mfano, mazao ya kwanza ya shamba kukomaa hutolewa kwa nyumba ya Bwana…(malimbuko) cha kwanza ni cha Bwana. Ni kweli imekuwa ni ngumu sana kwa watu wengi kuwa waaminifu katika suala zima la kutoa malimbuko kwa Bwana ambapo ni kosa kubwa na huzifukuza baraka za Bwana, maana Bwana  hubariki palipowekewa uaminifu. Na ni mara nyingi pia kwa wale walio waaminifu katika malimbuko wamekuwa ni watu wa baraka na kubarikiwa sana katika maisha yao ya kiroho na kimwili kwani wamelishika san agano la Mungu juu ya malimbuko yaani sadaka ya kuinuliwa. Tukisoma katika Biblia Takatifu kitabu cha Kumbukumbu la Torati (sheria) 12:11 (rejea hapo juu) MUNGU ANAJIBU

8. SADAKA YA KUTEKETEZWA
Aina hii ya sadaka ni sadaka ambayo ipo katika upekee wake, Mungu anafanya kama kutazama imani ya mwamini kwa njia ya kumtolea vile vinavyoweza kuumiza moyo wa mtoaji lakini yeye akiwa amewania kumbariki mtoaji kama alivyofany kwa Ibrahim. Tunasoma Mwanzo 22:1-2 “Ikawa baada ya mambo hayo mungu alimjaribu ibrahimu, akamwambia, Ee Ibrahimu! naye akasema mimi hapa.Akasema,umchukue mwanao,mwana wako wa pekee umpendaye,Isaka,ukaende zako mpaka nchi ya Moria,ukamtoe sadaka ya kuteketezwa huko juu ya mlima mmojawapo nitakaokwambia.” Na katika hili mtumishi wa Mungu Ibrahimu hakusita akamtoa mwana wake pekee na hata Mungu akaisikia sadaka ile naye akamjibu.

9.SADAKA YA SHUKRANI
Katika misingi ya kibiblia hii ni sadaka ambayo mwamini anamtolea Mungu wake kwa kuthamini na kushukuru kwa kile kitu/vile vitu Mungu amemfanyia katika wakati flani wa maisha yake (hata kama umepita katika magumu au raha ni vyema ukashukuru kwa kila jambo). Tunasoma katika kitabu cha Yeremia 40:29 “Nao watatoka miji ya Yuda…wakileta sadaka za shukrani nyumbani kwa Bwana”

TUNAPASWA KUTOA SADAKA WAPI?
Mahali sahihi pa kutoa sadaka ni KANISANI yaani nyumba ya Mungu… Kumbukumbu 12:5-7….”…Lakini mahali atapochagua BWANA, Mungu wenu, …maana ni makao yake,elekezeni nyuso zenu huko,nawe wende huko;pelekeni huko sadaka zenu…na dhabihu zenu , na zaka zenu….nadhiri zenu na sadaka zenu za hiari, na wazaliwa wa kwanza….”

KWANINI TUNATOA SADAKA?
a) Kutoa sadaka ni agizo la Mungu- kumbukumbu 8:6 Kutoka 25:1-2..”..Mungu akanena na Musa, waambie wana wa israeli kwamba wanitwalie sadaka……:
b) Kutoa sadaka ni kuonyesha utii kwa Mungu.. Unapotii unapata…kumbukumbu 28:1-8…. na usipo tii unapata haya… kumbukumbu 28:15-22. Pia soma Matendo 4:34-36…utaona jinsi watu wakitoa kwa uaminifu Matendo 5:1-10…utapata habari za anania na safira..
Kwahiyo, kutoa sadaka ni muhimu na pia kusaidia wajane na yatima ni muhimu..Unapomsaidia mtu mwenye shida haimaanishi kwamba umetoa sadaka bali umemsaidia kwahiyo kutoa sadaka kuko palepale… ukisoma MALAKI 3:7-10… Mungu anamfananisha mtu asiyetoa sadaka na mwizi… tena  anasema..”…mne niibia zaka na dhabihu,ninyi mmelaaniwa kwa laana; maana

No comments:

Post a Comment

KAZI KUU TANO (5) ZA IMANI KATIKA MAOMBI.

Bwana YESU atukuzwe ndugu zangu. Karibu tujifunze Neno la MUNGU. Uhusiano ni upendo unaozaa ushirikiano na mawasiliano kati ya pande m...