MWAKA WA NNE UPO DAR ES SALAAM (MJINI)
au upo jijini mwanza, arusha, mbeya na miji mingine.
Huna ajira nyingine zaidi ya kuhudhuria semina za akina Erick shigongo (Motivation Speakers) 'How to be #Rich' (Zimekupumbaza),
Unajua viwanja vikali vilipo, mitaa wanayoishi watu maarufu na habari za wasanii, hicho ndicho unakijua zaidi,
Unasema huwezi kuuza mandazi wala mkaa kwamba utajiaibisha lakini hapo ulipo huna chochote cha kumzidi huyo muuza maandazi na mkaa,
Ndugu zako wanakulaumu kwamba huwasaidii wakuombapo msaada na wewe hautaki kuyaweka wazi maisha yako maana unajua wazi ni aibu,
Unaanza kupata laana na mikosi bure kwa kujitakia mwenyewe.
Huana hata baiskeli, TOYO ya kuchora. (Huna mafanikio) umekalia kununua mashati ya gharama, high hills, vitop tu na unazeeka sasa, Mentors wako wanazidi kufanikiwa
(Wewe unafilisika kila siku)
Ndugu! wadogo zako uliowaacha kule kijijini kwenu/mkoani kwenu hawamjui Ruge wala Erick shigongo,
hawajui Motivation wala inspiration Quotes,
Lakini wana miliki Familia zao,
Wanaishi kwenye nyumba zao,
wanausafiri wa kutembelea,
Wana kazi zao zinazoeleweka hata kama za kujiajiri,
wanakula vizuri hawashindii kipande cha muhindi wa mia(100) au kipande ch muhogo na maji ya kandoro kama wewe.
Kwa sababu akili yako haijiwezi.
Unasubiri ruge Akuambie rudi kijijni (halafu nani asikilize clauds )
Au Shigongo akwambie Kalime matikiti au bamia (Muda wa kusoma gazeti LA IJUMAAA utapata wapi.) Hakuna wa Kukubadilisha Zaidi ya WEWE MWENYEWE
Usibague kazi ikiwa huna kazi, kazi ni kazi ilimradi tu iwe halali,
juhudi na ufanisi katika kazi
Ndio mafanikio yako.
Mjini patanufaisha macho yako tu kama hauna cha kufanya rudi nyumbani kajipange upya.
(Baada yakua umehamasishwa fanya kwa vitendo sio unaishia kumsifu muhamasishaji.)
#usiwazeUtajiri
#WazaKufanikiwa
#Halisi#
No comments:
Post a Comment