Saturday, 4 August 2018

Kwenye Maisha kuna AINA 4 za changamoto ambazo unaweza kupitia.

Kwenye Maisha kuna AINA 4 za changamoto ambazo unaweza kupitia.

Ya Kwanza: KUTOKANA NA MAKOSA YAKO.

Kuna changamoto huwa unapitia kutokana na makosa uliyofanya kwa kujua ama kutokujua. Ukishagundua hili hautakiwi kuendelea kujilaumu, jisamehe na angalia namna bora ya kuanza upya ama kurekebisha makosa kwa haraka.
Mara nyingi changamoto hizi zinahitaji WEWE MWENYEWE ndiye uchukue HATUA.

Ya Pili: KUTOKANA NA WANAOKUZUNGUKA

Kuna changamoto zinazotokana na watu wanaotuzunguka, inawezekana ikawa ni ndugu, wazazi, marafiki ama kazini. Mara nyingi changamoto hizi unaweza usiwe na uwezo wa kuzibadilisha Ila unaweza kutafuta mbinu za kuzipunguza, kuzikwepa ama kubadilisha mwitikio wako zinapotokea. Bila kujali nani anasababisha changamoto hii amua kufanya Kitu cha kukabiliana nayo, usiseme “itaondoka yenyewe tu”

Aina Ya Tatu: CHANGAMOTO ZA KUTUVUSHA

Kuna wakati changamoto zinakuja kwa sababu ya Ndoto kubwa tulizonazo. Changamoto hizi huisha kama utaamua kuacha unachokitafuta ila kama unataka kuendelea na zenyewe zinaendelea. Unachotakiwa kujua ni kuwa kupanda kwako juu ni matokeo ya kushinda changamoto zinazojitokeza.USIKIMBIE CHANGAMOTO,ZIKABILI.

Ya Nne: CHANGAMOTO ZA KUBADILISHA MWELEKEO KWA LAZIMA

Kuna wakati unashindwa kuendelea mbele kwa sababu ya Uoga wa kubadili mwelekeo wa maisha YAKO/Kufanya maamuzi magumu/Kubadilisha unachofanya. Kipindi hiki MUNGU huwa anatumia kwa kuruhusu changamoto fulani ili UCHUKUE MAAMUZI kwa LAZIMA au UBADILISHE MWELEKEO kwa lazima. Mara nyingi ukishapita baada ya Muda mrefu unakuja kugundua kuwa MABADILIKO yako YALIANZIA wakati wa Changamoto FULANI.

Changamoto ni sehemu ya Maisha USIRUHUSU IKUHARIBU, ITUMIE KAMA DARAJA. Umeshawahi kupitia yoyote kati ya hii?

No comments:

Post a Comment

KAZI KUU TANO (5) ZA IMANI KATIKA MAOMBI.

Bwana YESU atukuzwe ndugu zangu. Karibu tujifunze Neno la MUNGU. Uhusiano ni upendo unaozaa ushirikiano na mawasiliano kati ya pande m...