Swali: "Biblia inasema nini juu ya kushirikiana katika ngono kabla kuoana?"
Jibu: Pamoja na matendo mengine ya uchafu, kufanya kitendo cha mapenzi kabla kuoana kumekatazwa katika maandiko (matendo 15:20; warumi 1:29; wakorintho wa kwanza 5:1; 6:13, 7:2; 10;8; wakorintho wa pili 12:21; wagalatia 5:19; waefeso 5:3; wakolosai 3:5; wathesalonike 4:3; yuda7). Biblia inasisitiza kuepuka kitendo hicho kabla ya ndoa.hii ina maana ya kuwa ni dhambi kama ya uzinifu kwa kuwa hujaunganishwa na unayefanya naye kitendo hicho. Mapenzi baina ya mume na mke waliooana ndiyo mapenzi yanayokubalika mbele za Mungu (waebrania 13:4).
Kushirikiana katika ngono kabla ndoa kumeenea sana kwa sababu nyingi. Mapenzi yanastarehesha. Mungu aliyaumba hivyo. Anawataka wanaume na wanawake wafurahie kitendo cha ngono (ndani ya ndoa). Hata hivyo, lengo la msingi la ngono si starehe bali kuzaana tukaongezeke. Hivyo tunazuiwa kufanya kitendo cha ngono kabla ndoa ili tusijipatie watoto tusiowatarajia. Kama jambo hili lingezingatiwa, magonjwa ya zinaa na wamama wasioolewa na kuavya mimba na kadhalika kungepungua. Kujizuia kunaokoa maisha, kunalinda watoto wachanga na kuleta ladha halisi ya ngono pamoja na heshima kwa Mungu.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
KAZI KUU TANO (5) ZA IMANI KATIKA MAOMBI.
Bwana YESU atukuzwe ndugu zangu. Karibu tujifunze Neno la MUNGU. Uhusiano ni upendo unaozaa ushirikiano na mawasiliano kati ya pande m...
-
Bwana YESU atukuzwe ndugu zangu. Karibu tujifunze Neno la MUNGU. Uhusiano ni upendo unaozaa ushirikiano na mawasiliano kati ya pande m...
-
Bwana Yesu asifiwe… Imeandikwa ; “ Bali wote waliompokea aliwapa uwezo wa kufanyika watoto wa Mungu, ndio wale waliaminio jina lake; “Y...
-
Ni miaka mingi nimekuwa nikijiuliza swali hili, nitawezaje kumpenda Mungu kwa moyo wangu wote, kwa akili zangu zote na kwa nguvu zangu zote...

Nmebarikiwa sana mtumish wa Bwana na ujumbe huu
ReplyDelete