Swali: "Je, biblia inasema nini juu ya ushoga? Je, ushoga ni dhambi?"
Jibu: Biblia inasisitiza kila mara kwamba ushoga ni dhambi (mwanzo 19:1-13; mambo ya walawi 18: 22; warumi 1:26-27; wakorintho wa kwanza 6:9). Warumi 1:26-27 inatufundisha ya kwamba ushoga ni njia mojawapo ya kumkana na kutomtii Mungu. Mtu anapodumu katika dhambi na kutokuamini biblia inatuambia ya kwamba “Mungu huwaachilia” kutenda maovu zaidi ili wapate kujua ubatili wa maisha bila Uwepo wa Mungu. Wakorintho wa kwanza 6:9 inasema kuwa mashoga hawataurithi ufalme wa Mungu.
Mungu haumbi mwanadamu mwenye tamaa ya ushoga. Biblia inatuambia mtu huwa shoga kwa sababu ya dhambi. (warumi 1:24-27), na pia kwa sababu ya uamuzi wake mwenyewe. Mtu anaweza kuzaliwa na msukumo juu ya ushoga kama vile watu pia huzaliwa na msukumo juu ya fujo na dhambi nyinginezo. Hili halihalalishi dhambi yoyote inayofanywa na wanadamu. Je, mtu akizaliwa na msukumo wa hasira mbaya, ni halali aendeleze hasira zake mbaya? La, hasha. Hata kwa ushoga pia si halali.
Hata hivyo Biblia haiitaji dhambi ya ushoga kuwa ndiyo kubwa zaidi. Kila dhambi ni chukizo kwa Mungu. Ushoga ni mojawapo ya mambo yaliyoorodheshwa katika wakorintho wa kwanza 6:9-10 yatakayozuia mtu asiingie katika ufalme wa Mungu. Kulingana na Biblia msamaha wa Mungu juu ya shoga upo sawa na wa mzinzi, muabudu sanamu, muuaji, mwizi na kadhalika. Mungu tena aahidi uwezo juu ya kushinda dhambi, pamoja na ushoga, kwa wale wote watakao mwaminiYesu kristo kwa wokovu wao (wakorintho wa kwanza 6:11; wakorintho wa pili 5:17).
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
KAZI KUU TANO (5) ZA IMANI KATIKA MAOMBI.
Bwana YESU atukuzwe ndugu zangu. Karibu tujifunze Neno la MUNGU. Uhusiano ni upendo unaozaa ushirikiano na mawasiliano kati ya pande m...
-
Bwana YESU atukuzwe ndugu zangu. Karibu tujifunze Neno la MUNGU. Uhusiano ni upendo unaozaa ushirikiano na mawasiliano kati ya pande m...
-
Bwana Yesu asifiwe… Imeandikwa ; “ Bali wote waliompokea aliwapa uwezo wa kufanyika watoto wa Mungu, ndio wale waliaminio jina lake; “Y...
-
Ni miaka mingi nimekuwa nikijiuliza swali hili, nitawezaje kumpenda Mungu kwa moyo wangu wote, kwa akili zangu zote na kwa nguvu zangu zote...

No comments:
Post a Comment