Friday, 20 July 2018

SALA YA TOBA.

Bwana Yesu asifiwe…
Kwa ufupi.
Awali ya yote ni vyema ufahamu ; Bwana Mungu ameridhia kusikia maombi ya mtu mwenye dhambi katika eneo moja tu nalo ni kwenye maombi ya toba. “ Twajua ya kuwa Mungu hawasikii wenye dhambi; bali mtu akiwa ni mcha Mungu, na kuyafanya mapenzi yake, humsikia huyo. ” Yoh. 9:31. Hii inaonyesha kuwa si kwamba hawasikii kama kusikia kwa kawaida bali ina maana ya kwamba Hakuna majibu kwa yeye aombaye. Lengo kuu ni kumcha Mungu ili majibu na udhihirisho wake Mungu uonekane. Hivyo inaonesha ni muhimu kiasi kwamba milango iko wazi kwa mtu atubuye ili aweze kurejea. “ sala ya toba “ ni aina ya maombi ya kumrejesha mtu aliye dhambini amuelekee Mungu.
Mara nyingi maombi ya kurejeshwa yafaa mwenye dhambi / anayerejea aongozwe na mtumishi wa Mungu kwa kwa sababu hawezi kujiongoza mwenyewe. Hata hivyo imekuwa bahati mbaya leo, “maombi ya toba ” yamegeuzwa na kuwa jambo la kidini badala ya kuwa jambo la kiroho kwa sababu watu huomba kwa midomo bila moyo kuhusika. Fahamu jambo moja ya kwamba ; “ ni heri maneno ya moyoni kuliko maneno ya mdomoni tu ” usistajabu kusikia hivyo, ni msamiati tu huyo wenye maana ni afadhali sana maombi yatoke moyoni na yasitoke kwenye kinywa tu! Sababu waweza kuomba kwa kukariri bila moyo wako kuhusika na hapo ndipo pabaya kama nini!!! Lengo mama la ujumbe wa leo ni kukuwezesha uijue mfumo tu wa “ sala ya toba” ili mfumo /muundo huu ukusaidie si kwa kukariri bali kwa uelewa ili kusudi uweze kumuongoza ndugu yako sala ya toba, arejee kwa Bwana. Maombi yenyewe katika mfumo ni haya;
“ Baba katika Jina la Yesu, ninakushukuru kwa neema yako uliyonipa siku ya leo. Kwa neema hii, ninaomba unihurumie na unisamehe dhambi zangu zote nilizozitenda kwa kujua,na kwa kutokujua. Unisamehe dhambi zote zinazotokana na mawazo yangu, maneno , matendo yangu na kushindwa kwangu kutimiza wajibu. Ee Bwana Mungu, kutoka ndani ya kilindi cha moyo wangu ninaamua kukata shauri kuachana na maisha ya kale, maisha ya dhambi. Bwana Yesu, futa jina langu kwenye kitabu cha hukumu, andika jina langu kwenye kitabu cha uzima ; Ninamkataa shetani na mambo yake yote, nazikataa na hila zake, na mapepo yake nayakataa. Nakupokea Bwana Yesu, uwe Bwana na mwokozi wa maisha yangu kuanzia sasa na maisha yangu yote. Ee Yesu unisaidie. “
( Hiyo ni frame work, yaani ni picha tu, yafaa uione kisha maneno yako yatoke moyoni). Kumbuka ; sala ya toba / maombi ya toba yafaa;
  1. Yasichukuliwe au kuongozwa kidini yaani kwa kusaliwa vivyo hivyo yalivyo kwa kukariri.
  2. Yaongozwe na mtumishi wa Mungu ( mchungaji au kiongozi yoyote)
  3. Anayeongoza awe rohoni, pia anayeongozwa awe kweli amekubali mwenyewe bila shuruti / kulazimishwa. Asitishwe kwa lengo la kulazimishwa.
  4. Anayemuongoza lazima ahakikishe anamuombea mara baada ya maombi hayo na kumfunika kwa damu ya Yesu.
  5. Anayemuongoza ampe neno la matumaini kuonesha kwamba sasa amesamehewa dhambi zake zote, na asitende dhambi tena.
  6. Anayeongozwa yampasa aanze mara moja darasa la mafundisho ya uzima / kuukulia wokovu wake. N. K

No comments:

Post a Comment

KAZI KUU TANO (5) ZA IMANI KATIKA MAOMBI.

Bwana YESU atukuzwe ndugu zangu. Karibu tujifunze Neno la MUNGU. Uhusiano ni upendo unaozaa ushirikiano na mawasiliano kati ya pande m...