Tuesday, 6 February 2018

NENO LA LEO: MAPAMBANO NA FARAJA

BIBLE

*Bwana akamwambia Nuhu, Ingia wewe na jamaa yako yote katika safina ; kwa maana nimekuona wewe u mwenye _h a k i_ mbele zangu _katika k i z a z i h i k i_… MWANZO 7:1*

………Nuhu alikuwa amefuata kwa uaminifu maelekezo aliyoyapokea kutoka kwa Mungu. Safina ilimalizika kujengwa kila sehemu kama Bwana alivyoelekeza na vyakula vikihifadhiwa ndani yake kwa ajili ya watu na wanyama. Hapa tena , mtumishi wa Mungu alitoa *wito makini wa mwisho kwa watu*. Huku akiugulia kwa shauku ambayo maneno hayawezi kuielezea, aliwasihi kutafuta kimbilio wakati linapopatikana. Kwa mara nyingine walikataa maneno  yake na kuinua sauti zao kwa kejeli na kudhihaki. Ghafla ukimya ukatawala umati huu *uliokuwa ukifanya mzaha*. Wanyama.wa kila aina , wakali pamoja na wapole kabisa walionekana wakija kutoka kwenye milima na misitu na wakaelekea kwenye safina kwa utulivu. Kelele maana ya upepo uvumao ikasikika, na tazama, makundi ya ndege yakaja kutoka pande zote, idadi yao ilifanya anga kuwa jeusi na kwa utaratibu mkamilifu, walipita na kuingia kwenye safina. Wanyama *walitii amri ya Mungu* wakati watu wakikataa kutii. Walipoona wanyama wakitokea msituni  na kwenda kwenye lango la safina , na Nuhu akiwaingiza , walikuwa wamekwisha pinga ujumbe ambao Mungu alikuwa amewapatia kwa muda mrefu sana , walikuwa wamekwisha kataa kiasi kwamba…dhamiri zao zilikuwa zimefikia hatua ambayo hazingeweza kuvutiwa.

   ………Rehema ilikuwa imekoma kusihi kwa ajili ya jamii hii iliyokuwa na hatia . Wanyama wa porini na ndege wa angani walikuwa wameingia  mahali pa kimbilio. Nuhu na nyumba yake  walikuwa ndani ya safina na *”Bwana akamfungia*” … Lango lile kubwa , ambalo isingewezekana kwa wale waliokuwa ndani kulifunga, lilifungwa polepole kea mikono isiyoonekana. Nuhu akawa amefungiwa na wale waliokataa *rehema ya Mungu* wakawa wamefungiwa nje. Muhuri wa Mbinguni ulikuwa juu ya mlango huu; Mungu alikuwa ameufunga na ni Mungu mwenyewe ambaye angeufungua. Hivyo wakati Kristo atakapo koma *kufanya upatanisho kwa ajili ya wenye hatia , kabla ya kuja kwake kwenye mawingu ya mbinguni , mlango wa rehema utafungwa*. Neema ya Mungu haitaendelea kuzuia waovu na shetani atakuwa na udhibiti mkamilifu wa wale watakaokuwa wamekataa rehema. Watajaribu kuwaangamiza watu wa Mungu; lakini kama Nuhu alivyofungiwa ndani ya safina vivyo hivyo wenye  haki watalindwa kwa uwezo wa Mungu.

No comments:

Post a Comment

KAZI KUU TANO (5) ZA IMANI KATIKA MAOMBI.

Bwana YESU atukuzwe ndugu zangu. Karibu tujifunze Neno la MUNGU. Uhusiano ni upendo unaozaa ushirikiano na mawasiliano kati ya pande m...