Thursday, 18 January 2018
Imani ni . . . uthibitisho wenye kuridhisha wa mambo halisi ambayo hayaonekani.—Ebr. 11:1, maelezo ya chini.
Imani ya Kikristo ni sifa yenye thamani. Si wanadamu wote walio nayo. (2 The. 3:2) Hata hivyo, Yehova amemgawia kila mwabudu wake “kipimo cha imani.” (Rom. 12:3; Gal. 5:22) Wale wote walio nayo wanapaswa kumshukuru sana Yehova. Yesu Kristo alisema kwamba Baba yake wa mbinguni huwavuta watu kwake kupitia Mwana Wake. (Yoh. 6:44, 65) Kwa hiyo, kwa kumwamini Yesu mtu anaweza kupata msamaha wa dhambi. Hilo humpa tumaini la kufurahia uhusiano wa milele pamoja na Yehova. (Rom. 6:23) Je, tunastahili baraka hiyo nzuri ajabu? Kwa kuwa sisi ni wenye dhambi, tunastahili tu kufa. (Zab. 103:10) Lakini Yehova aliona jambo zuri ndani yetu. Kwa sababu ya fadhili zake zisizostahiliwa, alifungua mioyo yetu ili tupokee habari njema. Hivyo, tukaanza kuonyesha imani katika Yesu tukiwa na tumaini la kupata uzima wa milele.—1 Yoh. 4:9, 10. w16.10 4:1, 2
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
KAZI KUU TANO (5) ZA IMANI KATIKA MAOMBI.
Bwana YESU atukuzwe ndugu zangu. Karibu tujifunze Neno la MUNGU. Uhusiano ni upendo unaozaa ushirikiano na mawasiliano kati ya pande m...
-
Bwana YESU atukuzwe ndugu zangu. Karibu tujifunze Neno la MUNGU. Uhusiano ni upendo unaozaa ushirikiano na mawasiliano kati ya pande m...
-
Bwana Yesu asifiwe… Imeandikwa ; “ Bali wote waliompokea aliwapa uwezo wa kufanyika watoto wa Mungu, ndio wale waliaminio jina lake; “Y...
-
Ni miaka mingi nimekuwa nikijiuliza swali hili, nitawezaje kumpenda Mungu kwa moyo wangu wote, kwa akili zangu zote na kwa nguvu zangu zote...
No comments:
Post a Comment