Ndugu msomaji wangu, wakati huu ningepnda nikueleze maneno ya ufunuo yaliyotokea wakati Yesu anaandaliwa ili azaliwe na bikira Mariamu
Mathayo 1:18 KUzaliwa kwa Bwana wetu Yesu Kristo hapa duniani, kumeleta mambo yafuatayo:
i. Neema na fursa za kuzaliwa watumishi.
ii. Neema hii imefungua mlango dunia nzima ili neno hili litendeke.
iii. Fursa hii inasababisha wawepo watumishi wa kutosha katika shamba la Mungu aliye hai.
Kazi ya uweza wa Roho Mtakatifu;
Uweza wa Roho Mtakatifu ndiyo unaoleta neema na fursa hizi Luka 1:26-32, 35. Fursa hii ni kama ifuatavyo: inasiaidia kuleta watumishi wakubwa kupita mamba za ghafla. Hapa ni mahali pa ajabu ndugu msomaji, kuna wakati mama au mwanamke yeyote atakueleza kuwa pamoja na kutumia dawa za uzazi wa mpango, lakini anakuta amebeba mamba katika hali kushangaza. Mungu pia analeta watumishi kwa njia hii.
Sura ya Tatu
UTAJUAJE KUWA UTAZAA MTUMISHI
Luka 1:5-31, Mwanzo 6:10 Amuz 13:2,3 katika maandiko matakatifu ikianidikwa mtoto mwanamume au mwanamke, ujue kuwa ni alama ya kuwa utazaa mtoto mtumishi (NANI ANAELEWA KUHUSU MAANDIKO?)
Dalili au alama za mtoto mtumishi;
Ishara ya kukujulisha kuwa utazaa mtoto mtumishi ni kama ifuatavyo:
Akiwa tumboni wewe mama, utaanza tabia za pekee za kuwashangaza watu. Mfano: kuchukia dhambi katika namna ya pekee, vilevile utahisi namna Fulani zilizo katika tabia za watumishi hata wa enzi za biblia, inachipuka ndani yake. Aidha utapenda jambo fualani zuri kwa bidii mfano: kuimba, kuomba kumchezea na kumsifu Mungu, au kuepnda sana kusikiliza mahubiri au mafundisho. Inakuwa ni hali iliyozidi kawaida ya watu wengine. Mtoto atakapozaliwa sehemu ya tabia hizi atakuachia, na zilizobaki atazaliwa nazo.
Namna ya kumlea mtoto mtumishi:
Kwa watumishi wote ambao unajua dhahiri kuwa ndani ya malango yako umezaa watumishi zingatia yafuatayo:
i. Usimpige kichwani
ii. Unampomwadhibu, mjulishe kosa lake na biblia inasemaje kuhusu kosa hilo
iii. Usimtukane
iv. Usimwite majina machafu
v. Hakikisha hakosi ibada
vi. Tenga muda wa kuomba naye.
vii. Mfundishe neno la Mungu kwa usahihi, ili maneno ya uzima yakae kwa wingi mioyoni mwao
Sura ya nne
ULIMWENGU WA MWILI ULIKOMBOLEWAJE NA YESU?
Ili Yesu aweze kuifanya kazi ya ukombozi kwa ufanisi, ilimlazimu ajigawanye katika sura zifuatazo: Efeso 4:8-13
i. Sura ya Mungu aliye hai
ii. Sura ya Mwanadamu
iii. Sura ya Wanyama
iv. Sura ya Mimea
v. Kipimo cha miamba
vi. Kipimo au sura ya maji ya uzima
vii. Sura ya moto ulao (uteketezao)
Katika sura ya Mungu, Yesu anaitwa “Mungu mwenye nguvu” Isaya 9:6. Nguvu yake ya uungu inatuwezesha kupata, wokovu, msamaha na uwezo wa kuishi maisha matakatifu. Katika sura ya mwanadamu, anaitwa Mwana wa Adamu 1Timotheo 2:5-7. katika kipimo hiki alifanyika mwili, Yohana 1:14 ili atupe neema ya kuushinda mwili ili utu wa rohoni ukae vizuri ndani yetu 2 Korith 10:1-5 maana mwili na roho vinashindana sana. Ndiyo maana ndugu msomaji utakuta, ni vigumu watumishi kuugua magonjwa ovyo ovyo. Huu ni uthibitisho kuwa, kama utamtumikia Mungu kwa bidii una uhakika wa kuishi maisha marefu na afya njema.
Katika sura ya wanyama, Yesu anaitwa Mwanakondoo au simba wa kabila ya Yuda Ufunuo 5:1-7 Mwanakondoo anatabia za utii, upole na unyenyekevu. N ahii ni sehemu ya matunda ya Roho, yanayomwezesha mtumishi kusimama vema katika wokovu. Katika sura ya simba inadhihirisha kuwa ndani ya Yesu kuna nguvu na mamlaka ya kutawala na utisho, unaomwezesha mwanadamu kuutawala ulimwengu war oho, kwa mamlaka ya Yesu na kumdhibiti shetani na kazi zake.
Katika sura ya mimea, Yesu anaitwa Mzabibu. Hii ni sura inayoonyesha neema na faida za utumishi, kwamba chanzo cha nguvu za utumishi ni kutoka kwa Yesu. Na ili uishi maisha marefu inakupasa uwe mtumishi mwaminifu na hapo utahesabiwa kuwa tawi lizaalo matunda Yohaha 15:5-6. Usikae kanisani kihasara hasara maana, maisha yako yatakuwa mafupi. Kama Yohana anavyosema tawi lisilozaa hukatwa na kutpwa motoni.
Katika sura ya miamba anaitwa Mwamba wa Wokovu wetu. Hakuna linalomshinda. Yaani Yesu ni tegemeo letu.
Katika sura ya maji ya uzima, Yesu anaitwa maji ya uzima ya kuondoa kiu. Ina maana kiu za kila namna, mfano: kiu ya kusoma biblia, kiu ya maombi au kiu ya kumtumikia Yesu Kristo. Yohana 7:37-40.
Katika sura ya moto ulao, tunapata neema ya kuziharibu kazi za shetani kupitia moto wa Roho Mtakatifu.
Sura ya tano
UKOMBOZI WA ARDHI
Ndugu msomaji wangu, katika Yohana 3:16 inasema “Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu” Ardhi ni sehemu ya ulimwengu ambayo inahitaji kukombolewa. Mwanzo 3:17 Ardhi ililaaniwa baada ya Adamu kuihalifu ile amri iliyokataza wasile matunda ya mti uliyokuwa katikati ya bustani ya edeni Mwanzo 3:3. Ardhi inapolaaniwa laana inaingia umbali mrefu sana chini ya ardhi na ni zaidi ya mita 70 kwenda chini ya ardhi. Maana ardhi ya dunia imegawanyika mara tatu:
i. Eneo la juu – crust
ii. Eneo la kati – mantle
iii. Eneo la chini sana – core
Juu ya uso wa nchi au ardhi, kuna vitu vifuatavyo:
i. Mazao na mimea
ii. Mito
iii. Bahari
iv. Lulu
v. Madini
Laana ya ardhi inahusisha uchumi na utajiri wan chi kuathirika. Ndiyo maana matukio au janga la njaa huibuka, utakuta baadhi ya miji na mikoa katika nchi hushamuliwa na njaa kwa sabsbu ya ardhi kulaaniwa. Mfano nchi ya Tanzania imesheheni utajiri mwingi sana kama mito, bahari, misitu, mafuta, gesi na madini lakini mpaka leo uchumi wetu haufanani na utajiri uliopo katika ardhi ya Tanzania.
Nchi ya Israeli yenye ukubwa wa mita za mraba zaidi ya elfu ishirini ni tajiri kuliko sisi. Wataalamu wanasema mkoa wa Kilimanjaro ni mkubwa kuliko Israel. Lakini kwa kuwa ardhi ya Tanzania inatatizo la kiroho linalohitaji damu ya Yesu ndiyo maana wanaofaidi uchumi wa Tanzania ni wawekezaji kutoka mataifa ya kigeni. Waombaji wa Tanzania walione hili ili kuondoa laana ikaayo katika ardhi.Ardhi ikiwa na baraka ni lazima nchi itastawi kiuchumi na kibiashara.
Ndugu msomaji nadhani unakumbuka njaa iliyoipaata nchi hii (Tanzania) miaka ya 80 ambayo mpaka leo, vimelea vya athari zake bado zipo.
Jinsi mwanamke anavyohusishwa na uharibifu uliyoipata dunia Mwanzo 3:1-13
Uharibifu uliyoipata dunia au ulimwengu ulianzia kwa mwanamke (Eva) Ndiyo maana katika kitabu cha Isaya 7:14 unaeleza habari ya bikira kuchukua mamba na kumzaa mwokozi.
Ndugu msomaji fahamu hili, pale pale uharibifu ulipopita, wokovu nao ulipitia hapohapo. Maana Mungu aliye hai anamtumia sana mwanamke, na shetani naye anamtumia sana mwanamke hivyo usalama wa mwanamke ni wokovu na kumtumikia Mungu kwa bidii.
Mwanzo3:15-16 ofisi ya uadui iliwekwa na Mungu baba mwenyewe. Ndugu msomaji kitabu kijacho nitakueleza maneno ya unabii na mafunuo. Lakini kwa sasa endelea kufuatilia ufunuo uliyopo ndani ya Christmas au kuzaliwa kwa Yesu.
Isaya 27:1-8 ndiyo maana mwanamke anawindwa sana na shetani, kutokana na neno au andiko la Mwanzo 3:15-16. Hii husababisha jinsia ya kike kuwa hatarini wakati wa ujauzito. Kwanini Mwanzo 3:6 ndiye aliyeanza kula matunda ya mti wa ujuzi wa mema na mabaya.
Sura ya sita
Uongozi wa nyota
Ndugu msomaji wangu, maneno haya ya unabii wa nyota au mwongozo wa Mungu Mtakatifu kupita nyota ni maneno ya ndani sana nay a kifalme kwa mtumishi mwenye wokovu wenye kina, kimp na mapana na marefu. Vilevile yamesitirika au yamefichwa sana bila nuru ya ufahamu Efeso 1:18 Huwezi kuona chochote hapa. Na kwakuwa shetani anayajua tangu alipokuwa mbinguni, wakati vigumu kwa sasa kuyafundisha madhabahuni labda semina za ndani Isaya 14:5-20.
Mathayo 2:9 ‘Nyota waliyoiona Mashariki Ikawatangulia, hata ikaenda ikasimama mahali alipokuwapo mtoto” Neema ya kujua kuwa nota hii inaniongoza vizuri kuelekea alipo Yesu ni ufunuo wa pekee wa Roho mtakatifu. Ufunuo 1:10-20. Mamlaka ya utumishi huukupitia nyota, upo mikononi mwa Yesu mwenyewe. Ebrania 6:5 “Kulionja neno zuri la Mungu na nguu za zamani zijazo” Ayubu 38:7 Mbali na unabii, nyota hulet vipaji vya uimbaji kutoka mbinguni. Ayubu 9:7-11. Maneno mengi matukufu ya kutumishi yamefichwa katika nyota. Vileviel hatari iliyopo nikwamba na shetani naye anao uwezo huu katika maneno ya nyota Ufunuo 9:1, 8:10, Isaya 14: 12-13 ndiyo maana watumishi wengi wanogopa kufundisha haya maneno. Maana ni kama vile Farao na Musa walivyokuwa wakonyeshana miujiza inayofanana. Kutoka 7:8-13 wakati wa kuzaliwa Yesu nyota zilihusika sana katika kuleta ujumbe.
Hesabu 24:17-19 Vilevile Mungu alipowaumba wanadamu aliwapa kitu chema kikaacho ndani kwa surea ya nyota ili kuhifadhi baraka zifuatazo:
i. Baraka za fedha
ii. Baraka za utumishi
iii. Kustawi kiutumishi
iv. Kufanikiwa na kustawi kijamii.
Isaya 61:1-4, 10:27 Ndiyo maana machawi anapomloga mtu, hushambulia na kuharibu nyota, ndipo nuksi, mikosi, balaa na bahati mbaya huanza kumwandama mtu huyo. Hivyo huduma ya ukombozi wa kuondoa laana, ilnalenga kumfungua mwanadamu eneo hili, ilipoharibika nyota yake.
Aina za nyota: Hesabu 24:17-19
i. Nyota ya utawala
ii. Nyota ya ukoo
iii. Nyota ya kabila
iv. Nyota ya utumishi
v. Nyota ya mafanikio
vi. Nyota ya kifalme Kumbukumbu 33: 13-14
Ufunuo 4:3 Jiwe la yaspi
Jiwe la yaspi ni kito cha thamani kinachong’aa kiwekwacho ndani ya nyota ya utmishi. Ndugu msomaji kama nilivyokueleza hapo awali, hii ni sehemu ya maneno ya kiwango cha juu sana kiroho, na siyo rahisi kukufundishwa katika vyuo vya biblia isipokuwa Roho Mtakatifu akufundishe.
Jiwe la yaspi linaifanya nyota ya utumishi ikae imara ndani ya nafsi ya mwanadamu. Hili jiwe la yaspi linamfanya mtumishi awe na bidii na juhudi katika utumishi kwa kiasi cha kushangaza
Sura ya saba
Maandalizi ya kuzaliwa Yesu Luka 1:13-18
Maandalizi ya kuzaliwa Yesu Kristo yalianza ulimwengu war oho. Mungu baba aliituma roho ya Eliya irudi tena Luka 1:17 ili kutayarisha ujio wa Yesu. Mathayo 17:9-13. Ile roho ya Mungu mtakatifu uliyotumika na Eliya, ilirudi na kuzaliwa ikiwa ndani ya Yohana mbatizaji. Ukisoma 1Falme 1:8 na Mathayo 3:4 utapata uthibitisho kuwa ile roho iliyotumika na Eliya, ilirudi tane akazaliwa Yohana Mbatizaji. Ukiangalia katika maandiko Luka 1:39 – 44, unakutana na neno la pekee, Mariamu alipoingia nyumbani mwa Zakaria, babaye na Yohana, mawasiliano ya ulimwengu war oho yalifanyika. Alipomsalimia tu Elizabeth kitoto kichang tumboni mwa Elizabeth kikaruka kwa Shangwe Luka 1:44 Wakati huu, Yesu alikuwa tumboni mwa Mariam, na Yohana alikuwa tumboni mwa Elizabeth. Lakini huwa roho zinatambuana maana zote zinatoka mbinguni.
Jinsi Roho ya Yesu ilivyokuja Luka 2:8-13.
Ililetwa na jeshi la mbinguni katika hali ya utukufu sana Luka 1:13. Yesu alipokuwa anaingia tumboni mwa Mariamu ilikuwa ni kimiujiza kama ifuatavyo;
i. Mwili unaanza kuumibika
ii. Nafsi inakuja mwezi wa tatu au wakati wowote, kama vile Mungu aliye hai apendavyo.
iii. Mwezi wa nne ndipo roho itakayotumika inaingia.
Mungu aliye hai anapoamua kuwa roho Fulani izaliwe dunaiani, anachagua aina ya mwanaume na mwanamke wa kumzaa mtoto huyo. Mfano Yusufu baba wa kimwili wa Yesu anatoka ukoo wa Daudi, kwa hiyo ni ukoo wa kifalme, kikuhani, na kinabii. Mariamu alikuwa anatoka ukoo wa Walawi inamaana ni uko wa kikuhani, kitume na kiinabii.
Hii ni siri ya pekee iliyopo ndani ya vitabu vya injili, ndiyo maana wakati mtu anaoa, huwa kwa kawaida anatumwa mshenga ili kwenda kuangalia na kuchagua aina ya mke, mwenye sifa njema kuanzia uliwmengu war oho na ulimwengu wa mwili.
Kwa wakatu huu wa sasa
Katika uzazi wa sasa, neno hili huweza kutendwa na Roho Mtakatifu, akitumia uweza wake ili kuleta watumishi hodari duniani na kuleta pia watumishi watakaotumika na karama au vipwa vikubwa vya Roho Mtakatifu. Swali kubwa ni utajuaje? Jibu, mtoto atakayezaliwa, atakuwa wa pekee.
Tafsiri za majina na hatari iliyopo
Ndugu msomaji ningependa kukushirikisha ufunuo wa Roho mtakatifu katika vizazi na majina hapa duniani na athari zake zinazoanzia ulimwengu wa roho. Luka 1:13 Jina la Yohana lilitoka mbinguni na lililetwa na malaika Gabriel Luka 1:19
Unapozaa mtoto, uwe makini au mwangalifu wakati unachagua jina la kumpa mtoto. La sivyo inawza kuwa balaa au laana ya kutisha. Maana kila jina lina maana. N aile maana ndiyo itakayokuwa sehemu ya maisha ya mtoto uliyemzaa.
Hatari iliyopo
Hata kama jina ni la kibiblia, chunguza kwanza lina maana gani? Na mwenye hilo jina aliishi maisha gani? Maana kuzaliwa kwa Yesu, vilevile ilikuwa na lengo la kufanya ukombozi katika majina waliyo nayo wanadamu (Yoh 3:16)
i. Samsoni, alikuwa mnadhiri wa Mungu, na alizaliwa ili kuwakomboa Israel na mkono wa Wafilisti Wamuzi 13;1-14. Lakini mwisho wa Samsoni ulikuwa mbaya sana. Alioa kinyume na utaratibu ambao Mungu aliwaamuru Israel. Baadaye alikufa kifo cha kusikitisha. Wamuzi 16:1-25
ii. Yefta au Yeftha, mgileadi alikuwa mwana wa manamke kahaba Wamuzi 11:1-3. Ni kinyumba au ukoo wenye asili ya ukahaba, kwa hiyo unapomchagulia mtoto jina hata kama ni la kibiblia uwe makini sana.
iii. Reubeni ni mtoto wa kwanza wa Yakobo, lakini alilaaniwa na babaye kwa kuwa alizini na suria la Yakobo Mwanzo 49:2-4. N ahii ni laana ya uchafu au uzinzi na mmoja wa mama zake Reubeni ukithubutu kutumia jina hili uwe makini usije ukaingiza laana au mashambulizi ya kipepo katika ukoo wako.
iv. Simeoni ni mmoja wa watoto wa Yakobo, wenye hasira mbaya na roho ya uuwaji. Hii ni jamii ya watu ambao kila mara huusika katika uhuni, ukatili na mauwaji ya kutumia kisu au panga. Hata hapa Tanzania yapo makabila yenye tatizo hili Mwanzo 49:5-7 ndiyo maana ndugu msomaji, sio kila kabila ni la kuoa au kuolewa nalo maana utapata uzao wa majambazi au wakora. Ni vizuri kuchunguza ukoo ambao mtoto wako anataka kuoa, au kuolewa. Lakini maombi ni dawa. Mwanzo 28:1
v. Yakobo alichukuwa mbaraka wa ndugu yake kwa hila Mwanzo 27:1-36. Yakobo maana yake ni mtu mwongo. Ndiyo maana jina hili la Yakobo lilibadilishwa na kuitwa Israel. Mwanzo 32:24-28. Jina Israel lilitoka mbinguni
Kuzaliwa kwa Yesu hapa duniani, kumeleta ukombozi wenye ufunuo wa pekee hasa kuhusu majina waliyo nayo wanadamu yabadilike. Jina alilonalo mwanadamu yeyote huweza kusababisha baraka au mashambulizi ya nguvu za giza. Roho mtakatifu akusaidie ndugu msomaji kuelewa na kupata mafunuo yenye kina, kimo, mapana na marefu ili uwe na amani ya kutosha. Kwa kuwa kuna amani ambayo hutoweka kutokana na ujinga wa kutokuyajua maneno ya uzima ya Mungu aliye hai kutoka ulimwengu wa roho.
Ayubu 22:21 kwa hiyo ndugu msomaji wangu uwe makini sana. Usiache kuomba Mungu ili akupe ufunuo zaidi katika siri za ufalme wa mbinguni.
Neno la kuzingatia ni hili, ndugu msomaji wangu, kitabu hiki nimekiandika kwa ufunuo niliopewa na Roho Mtakatifu ili niwaletee watumishi wake. Yaweza kuwa maneno mapya kwako na vilevile vyuo vingi vya biblia hawayafundishi. Lakini wewe umepata bahati iliyo njema sana. Fundisha watu wake au kanisa unalochunga ili wajue vizuri maneno ya kiroho, kwa aida ya mwili wa kristo Yesu.
Sura ya tisa
Faida za damu ya Yesu
Ndani ya damu ya Yesu kuna faida kubwa na nyingi sana. Maana Yesu ni lango la kuingia mbinguni, alifungua lango la Ibrahimu ili sisi tupate nafasi, akafungua lango lingine liitwalo kanisa.
Sheria za damu na ulimwengu wa Roho Ebrania 9:18
Ni sheria katika mahakam za mbinguni, ulimwengu war oho huwa unadai damu. Damu inapomwagika unasaini mkataba na roho. Kwa nini? Ni kwa kuwa damu inaongea. Mwanzo 4:10-12, Ebrania 9:15-18 Nguvu tuliyo nayo katika wokovu inatokana na agano lililofanyika kupita damu ya Yesu. Ebrania 10:1-12 Ndiyo maana wachawi hutambika kwa kutoa kuku, mbuzi au ng’ombe ili wapate yale wanayoyatafuta katika ulimwengu wa shetani. Na sisi tuliookoka, siri ya nguvu zetu imo katika damu ya Yesu. Kambi ya Yesu nguvu yetu ni damu yake, na kambi ya shetani na wao hutumia damu. Nidyo maan akanisa kupitia damu ya Yesu limebeba siri ya uzaliwa wa kwanza. Mfano (Rum 8:29);
i. Uongozi
ii. Baraka.
iii. Hatma njema
iv. Nuru
v. Chumvi
vi. Utawala
vii. Mbeba nguvu za maongezeko.
Dunia inatakiwa isaidike kupitia kanisa la Kristo hapa duniani. Haya yote yanafanikiwa, kupitia uweza wa jina la Yesu. Hii ndiyo faida ya kuzaliwa Yesu hapa ulimwenguni, ili kuukomboa ulimwengu.
Mjumbe Kutoka Mbinguni;
Malaki 3:1 “Angalieni namtuma mjumbe wangu naye ataitengeneza njia mbele yangu” Mjumbe aliyetumwa kuitengeneza njia kwa ajili ya ujio wa Yesu alikuwa ni Yohana Mathayo 3:1-4.
Siri ya Yohana Kutoka Ulimwengu wa Roho
Yohana 1:6-9 Neno la ajabu hapo ni hili, ya kuwa “Mtu ametumwa kutoka kwa Mungu” hapa kuna siri yenye ufunuo. Maana angesema kuwa “ametumwa na Mungu” ingepunguza maswali, lakini inasema ametumwa kutoka kwa Mungu inamaanisha kuwa, Kuzaliwa kwa Yohana ilikuwa ni kwa kusudi la Mungu ili kumnyooshea Yesu mapito.
Roho ya Yohana;
Luka 1:11-17 Inaandikwa kuwa “Naye atatangulia mbele zake katika roho ya Eliya” anaposema palikuwa na mtu ametumwa kutoka kwa Mungu Yohana 1:6 inamaanisha kuwa Roho ya Mungu mtakatifu iliyotumika na Eliya ilitumwa tena duniani. Nidyo maana maandiko yamesema “Plikuwa na mtu ametumwa kutoka kwa Mungu” kwa kuwa Eliya, kama tunavyofahamu, alitwaliwa na magari ya farasi wa moto kwenda mbinguni. Lakini kiroho, alikuwa hajamaliza kazi, ndipo Mungu aliamua kuituma tena roho hii ili kutengeneza njia kwa ujio wa Yesu.
2Falme 2:9-12 Na hii inadhihirisha kuwa Eliya na Yohana ni miongini mwa wanadhiri (watumishi maalumu wenye agano Fulani na Mungu mtakatifu) ambao kuwepo kwao duniani ni kwa kusudi pekee la kitume na kinabii. N uwepo wao duniani ulileta udhihirisho na utiisho wa Mungu aliye hai yaani Yehova.
Ujumbe kwa Watumishi Wote
Wito kwa watumishi wa Afrika na Tanzania ni huu; Kumbukeni kuwa msingi wa leo umejengwa jana na msingi wa kesho unajengwa leo. Neno kubwa analowadai Roho mtakatifu ni upendo, umoja, mshikamano, kuheshimiana na kutambuana. Kwa kukosekana haya yote imesababisha matabaka, ugomvi, mashindano yasiyo na maana, kushambuliana na majivuno. Katika sra hii kanisa la Tanzania haliwezi kustawi kama apendavyo Yesu aliyewaita. Zaburi 133:1-3 kila mmoja atembee katika ramani ya utumishi na wito wake, huku mkiomba hekima na mwongozo sahihi wa Roho mtakatifu.
Namna ya kuinua Huduma za Watumishi Chipukizi:
Neno hili limekuwa gumu sana ndiyo maana ikasababisha kuibuka huduma au makanisa mengi kuanzia mwaka 1988 mapaka 2009. Kumekuwa na tatizo la watumishi kuatamia madhabahu kama kuku anavyoatamia vifaranga vyake. Unakuta mtumishi wa kanisa (Askofu, Mtume) anahudumu madhabahuni toka jumapili hadi jumapili, hili ni kosa la kiufundi au ni roho ya ubinafsi. Vijana waliyo makanisani wanakosa mtu wa kuzichochoa huduma chipukizi ndani yao. Ndiyo maana wanakimbia na kwend akuanzisha huduma mpya. Vijana wa jinsia zote, wenye huduma chipukizi wapewe nafasi ya kusmama madhabahuni, imarisha huduma zao na kuwakosoa kwa upendo. Jitahidi sana wewe askofu au mchungaji usiwe na roho ya wivu mbaya au roho ya kwanini. Wazee wa kanisa ulio nao wapewe nafasi ya kuhubiri, hata jumapili siyo mapaka uumwe au uwe na dharura ndipo uachie madhabahu, bali wape nafasi vijana kwa wazee. Zab 119:161. kwa kufanya hivi furaha itatawala kanisani kwako. Hata ukiondoka duniani, utaacha alama na utakuwa mfano mzuri wa kuigwa.
Kutegemeza Wanao Hudumu:
Pamoja na wewe Zab 119:49-50 katika makanisa mengi vijana hujitoa kutumika kwa bidii mfano:
i. Praise team (waimba sifa)
ii. Kwaya
iii. Mashemasi.
Watu hawa usiwasahau hasa kifedha. Angalia hali halisi unapotaka kijana asikosekane kanisani ka wiki nzima ili kusimamia huduma Fulani, au uimbaji. Andaautaratibu mzuri wa kifedha ili waweze kujikimu kimaisha. Sidhani kama inahitaji kukupa andiko ila uwe makini ufuatilie na uyafanyia kazi haya yote, maana kuwa mwalimu na mtumishi mzuri ni pamoja na wewe kukaa chini na kuwasikiliza wenzako, Zab 118:15 wakiwemo watu wa nyumbi kwako Zaburi 80:11
Tafuta Chakula cha Uzima cha Kutosha zaburi 81:10
Hatari iliyopo ni hii, kuna wakati unakuja ambapo watu hawatavutika na majengo mazuri au vifaa vya muziki vya thamani. Ila watu watataka uwafundishe maneno ya uzima ya kushibisha roho zao. Tofauti na hapa watu watakukimbia. Na kitu wanachohitaji watu ni wewe kuhubiri au kufundisha maneno ya uzima yenye; chumvi, asali na mafuta na siyo kuhubiri maandiko. Maana ufunuo wa Neno ndiyo kitu cha muhimu sana. Usione aibu kwenda kujifunza kwa watumishi wenzako. Maana katika utumishi kuna yafuatayo:
i. Kuitwa,
ii. Kutayarishwa
iii. Kutumwa
Zaburi 91:45, 119:105 sas fahamu alama hizi za nyakati ili ikuwezeshe kujitambua wewe mwenyewe nafasi uliyo nayo. Na umtambue mwenzako na kumweshimu.
Sura ya Kumi na Moja
Namna ya Kutunza Waumini Wenye Huduma au Karama:
1Korontho 12:1-11 Kuchunga washirika wenye huduma au karama mbalimbali, ni neno gumu sana, ambalo linawasumbua watumishi wengi sana. Maana wengi hawajafundishwa walipokuwa vyuo vya biblia. Maandiko hayatoshi peke yake katika eneo hili, bali hekima ya Roho Mtakatifu inahitajika sana. Ni rahisi kuchunga waumini elfu hamsini wasiyo na karama yoyote kuliko, waumini saba wenye karama mbalimbali za RohoMtakatifu. Ili uweze kuwachunga inakubidi uwe na yafuatayo:
i. Nuru ya ufahamu
ii. Karama ya kupambanua roho
iii. Karama ya hekima
iv. Uwe umepevuka kiroho.
Maana ufunuo na siri ya kuzaliwa kwa Yesu imefungua mlango ili Roho mtakatifu aweze kuchukua hatamu na kulifikisha kanisa katika kweli yote. Yohana 16:12-16
Namna ya Kumtuliza Mtu Aliyefurika na Roho Mtakatifu:
Unapotaka kumtuliza mtu aliyefurika na Roho Mtakatifu ufanye yafuatayo;
i. Hakikisha umejitakasa
ii. Omba kibali cha Roho Mtakatifu
iii. Hata kama wewe ni Askofu, mtume au mchungaji, nenda kwa unyenyekevu wa hali ya juu.
iv. Mshike mgongini taratibu
v. Ukiwa umezama kiroho, sema Amen! Mara nne
vi. Kama hajanyamaza, endelea kusema amen mpaka atatulia.
vii. Kama hali ya kufurika imesalia kidogo haitoki yote, mpe glasi moja ya maji ya kunywa, ndipo atatulia. Mwanzo 1:2 Na kurudi katika hali kawaida.
Epuka Yafuatayo:
Unaposhughulika na mtu aliyejaa Roho mtakatifu. Epuka yafuatayo:
i. Dharau
ii. Kiburi
iii. Epuka kumshika utosini na kuanza kumkemea, unaweza kuabishwa na Roho Mtakatifu mwenyewe kwa namna yeyote.
No comments:
Post a Comment