Wednesday, 15 November 2017

UHUSIANO WA KARAMA ZA HUDUMA TANO NA WAZEE WA KANISA.

Uhusiano Wa Karama Za Huduma Tano Na Wazee Wa Kanisa.
1. Mtume –Huhitajika ili Kuongoza.
2. Nabii – Huhitajika ili Kuonyesha mwelekeo
3. Mwinjilisti - Huhitajika ili Kukusanya au kuvuna.
4. Mchungaji – Huhitajika ili Kulinda au Kutunza.
5. Mwalimu – Huhitajika ili Kujenga msingi / kufundisha.
Mtume na Mwinjilisti – huhudumu pia mbali na kanisa la nyumbani-Huduma za kimisheni.
Nabii na mwalimu – huweza pia kusafiri, lakini wanayo kazi maalumu sana nyumbani.
Mchungaji huhudumu kanisani, lakini aweza kwenda katika huduma za kimisheni.
Mamlaka Ya Wazee Wa Kanisa.
Mandiko hayaonyeshi uhusiano a moja kwa moja kati ya Huduma tano na wazee wa kanisa.
Zipo kweli kadhaa zinazo zinazo onyesha uhusiano wake.
1. Agano Jipya halitaji kamwe neno huduma tano. (Ila Efe.4:11; 1Kor. 1Kor.12:)
a. Ni karama za huduma sio ofisi (ofisi ina maana watu huhusika katika kupiga kura au kuchagua na
kisha kuwasimika viongozi au mawakili katika huduma fulani) b. Ni karama za maongozi / maangalizi.
2. Zipo osisi za aina mbili tu katika Agano Jipya (Fil.1:1)
a. Wazee wa Kanisa.
b. Mashemasi. (1Tim.3:1-15)
3. Maandiko Hutaja tu wazee “Kusimikwa” kwa maombi kufunga na kuwekewa mikono.
4. Wazee hushika nafasi ya wajibu na mamlaka katika kanisa. (1Tim. 5:17, Mdo. 20:17; 21:18-19; 11:30)
5. Baadhi ya Walipo katika huduma tano huweza kusimikwa kuwa wazee wa kanisa.
a. Mchungaji ndiye Mkuu wa wazee wa kanisa- “Mzee kiongozi”.
b. Baraza la wazee wa kanisa latakiwa liwe na Mchungaji, Nabii, na Mwalimu- ili liwe na utendaji mzuri.
i. Mchungaji anatakiwa awe na
1. Moyo wa kichungaji
2. Maono ya kiunabii
3. Hekima ya mwalimu

c. Hata Mtume, Mwinjilisti, Nabii au Mwalimu lazima awe na kanisa la Nyumbani atokako!
TABIA ZA MASHEMASI – [1Timotheo 3:8-13.]
1) Ujazo wa Roho Mtakatifu
2) Mwenye upendo kwa kanisa
3) Kuwa na msimamo – mwenye kauri moja na ile ya Neno la Mungu, mchungaji pamoja na wazee wa kanisa.
4) Mwenye uamuzi mzuri, bila ya kigeugeu.
5) Wasio na tamaa wala choyo (kuhusu pesa na mali)
6) Wenye imani na uwezo wa kuitetea imani.
7) Wenye dhamiri safi
8) Wasiio na hatia – wenye maisha safi.
9) Wenye ndoa takatifu (mme na mke mmoja).
10) Wawezao kufundisha na kuelekeza wengine.
11) Kukubalika / kutokulaumika
12) Wenye kiasi(kujitawala) na busara
13) Wenye kufuata utaratibu (mpangilio/ratiba na kanuni)
14) Ukarimu (ukaribishaji)
15) Wenye kujua kufundisha (mwalimu)
16) Si mtu wa kujadiliana (Mbishi)
17) Mwenye kuisimamia nyumba yake vizuri – mwenye sifa nzuri nyumbani.
18) Asiwe mchanga kiroho.
19) Mwenye ushuhuda mzuri kwa wasioamini pia.
20) Mwenye kupenda kutumikia na si kutumikiwa.

No comments:

Post a Comment

KAZI KUU TANO (5) ZA IMANI KATIKA MAOMBI.

Bwana YESU atukuzwe ndugu zangu. Karibu tujifunze Neno la MUNGU. Uhusiano ni upendo unaozaa ushirikiano na mawasiliano kati ya pande m...