Thursday, 19 October 2017

Kuna baadhi ya vijana ambao wanatamani kuingia katika ndoa lakini kuna baadhi ambao wanasema kwamba ,,bado nipo nipo kwanza,, na hii ni kwa wanaume na wanawake,,katika uchunguzi wangu nimeona kwamba vijana wengi wanachelewa kuoa au kuolewa kutokana na kuogopa majukumu kwani anaona bado hajajipanga vizuri, wengine ni kushindwa kujiamini anaogopa kuingia kwenye ndoa kwa hofu ya kukosa uhuru anaoutaka katika mambo yake ya starehe,,

 Wengine kutokana na kulazimishwa na wazazi kuoa au kuolewa na wachumba watakaowachagua wao  na kikubwa pia ni hali duni ya maisha kwani kuna mwingine anatamani kuoa lakini anaona kipato chake ni kidogo kufanya hivyo.

 Jamani mapenzi ni zaidi ya kipato ulichonacho kwani unaweza kuamua kuingia kwenye ndoa na huku mkiwa katika hali duni ya maisha,,baadae mkafanikiwa kwa juhudi zenu binafsi na kwa ushirikiano kati ya mke na mume muhimu ni kujiamini na kujitambua.....

Sababu nyingine kwanini wanaume wengi wanachelewa kuoa 

Mungu awaponye wanaume katika hili ndoa ni baraka 


1Wakorintho 7:8-9 "Lakini nawaambia wale wasiooa bado, na wajane, Ni heri wakae kama mimi nilivyo. Lakini ikiwa hawawezi kujizuia, na waoe; maana ni afadhali kuoa kuliko kuwaka tamaa".

Ni jambo la kawaida siku hizi kuona Kijana wa kiume anakomaa hadi kidevu bila kuoa, ukiwauliza wanatoa sababu ambazo kwa kweli sio za Msingi, na bahati mbaya sana wanaishia kuwa na ndoa za masaa kwa ajili ya kukidhi TAMAA zao za mwili. Utasikia wakisema "Jamaa kachukua bonge la Mzigo! ", huku binti akifikiri amepata mume kumbe yupo kukidhi TAMAA.

Kuna sababu nyingi zinazowafanya wachelewe kuoa, baadhi ni hizi:
KUTOJIAMINI AU UOGA WA MAISHA - Vijana mjiamini, ukiwa na uwezo wa kupanga chumba, kupata chakula, kuvaa na mahitaji mengine madogo yanatosha KUOA. Nyumba, Magari, Mashamba, flat screen, Masofa ya kifahari n.k, havina mchango katika kuanzisha ndoa yenye furaha. Mkipata mali pamoja ni vizuri zaidi kuliko mmoja akute kila kitu kipo, zitaishia kuwa ni mali za mtu mmoja.

SEMENI UKWELI - Wengi wanajifanya kuwa wana uwezo kifedha kumbe hamna kitu, Binti akifuatilia anagundua wewe sio mkweli, anakudharau, uwe kweli, weka mambo yako wazi, itakujengea kujiamini na kuaminika na mwenzio. Wengine ni waoga kutangaza nia, wanaishia kusema "Nampenda sana yule Binti" wenzao wakitangaza nia, wanaanza kuzusha "Yule tayari nilisha onja kumbe muongo", kazi yao ni kuwaharibia sifa mabinti. Wengine, kamwambia tu Binti nakupenda, hata hajapewa jibu, tayari mji mzima wanajua, akija kukataliwa inakuwa aibu.

KUTOWAAMINI MABINTI - Muda wote wana mtazamo HASI "Negative thinking" juu ya mabinti, kwa sababu alimharibu mmoja, basi kila Binti anayemuona anamdhania sio mwaminifu, anaishia kusema HAPA SIONI wa kuoa. Utakuta mabinti waaminifu wapo ambao hata mende hawajawapitia, lakini vijana wanaishia kusema hawaoni. Kitu cha ajabu unashangaa kaenda KUZOA yeyote, mbali ambako hawajui, na wengine wanajichnganya hadi wa Imani tofauti. Vijana! Tulieni, Oa huyo unayemjua vizuri, utaishia kuoa hadi mshirikina.

KUTAFUTA BINTI MZURI WA VIWANGO - Kuna Vijana wengi wanajidanganya wakidhani wasichana wazuri kuliko wote ndio wanafaa kuoa, kuna wengi walitumia kigezo hicho walijuta kama sio ndoa kuvunjika. Utasikia vijana wakisema "Reception yake imetulia" huyu ndiye wa kuoa. Wanaanza kugombania na mwishowe wote wanakosa, baada kugundua ni kidumu cha Wenye nazo. Sikiliza; Mungu ameumba kwa namna ya ajabu sana, kila mtu amempatia kitu ambacho mwingine hana, hivyo anayekufaa na kukidhi hitaji lako la Ndoa ni Mungu peke yake anayejua.

Ndio mana kuna usemi usemao "Uzuri wa Mtu uko machoni pa Mtu anayemuona Mzuri", vijana wanatafuta, figure eight, miguu chupa ya bia, macho ya panzi, rangi ya chungwa, maziwa embe dodo nk, hayo yote yanawafanya vijana wengi kuchanganyikiwa na kubaki wanahaha bila mafanikio. Rafiki kuna watu hawana sura wala rangi au umbile zuri, lakini Mungu amewapa ziada vingine ambavyo ukioa hutasikia la Mtu. Ndio utasikia watu wanasema "Hivi huyu kampendea Nini? " siri anaijua yeye. Wengine wanasaka mabinti wasioguswa na mwanaume, bila kujali kuwa wao wameshaguswa, na huku wanamuomba Mungu - kijana mhuni anataka asiyemhuni - huo ni Utapeli.

UHUNI, vijana wasio waaminifu kwa Mungu wanasukumwa na tamaa za mwili, na kwa sababu wanategemea akili zao,  hawawezi kustahimili msukumo wa mwili, wanaishia kuoa kimtindo, anaoa usiku na asubuhi talaka. Hao ndio wanaishia kutangaza Uchumba kwa kila Binti anayemuona, na mabinti wanaishia kubwagwa mara baada kutoa TUNDA, kwa sababu ya kutojua tofauti kati ya TAMAA na UPENDO wa dhati wenye lengo la Ndoa.

Ukiwa mwaminifu Mungu atakupatia bikira safi, mwaminifu utakaye dumu naye milele.

VIJANA WA KIUME MTEGEMEENI MUNGU NAYE NI MWAMINIFU ATAWAPATIA WAKE MTAKAOFANANA NAO.

 Ubarikiwe unapochukua hatua.

No comments:

Post a Comment

KAZI KUU TANO (5) ZA IMANI KATIKA MAOMBI.

Bwana YESU atukuzwe ndugu zangu. Karibu tujifunze Neno la MUNGU. Uhusiano ni upendo unaozaa ushirikiano na mawasiliano kati ya pande m...