Uamsho wa kiroho ni badiliko rahisi la ndani ya ufahamu wa mtu.
Uamusho wa kiroho sio maendeleo yenye mwisho. Ni Uhakika unaoonyesha matendo na mawazo ya mtu mwenye mwanga halisi wa Mungu kulingana na mitazamo yake.
Uamusho wa kiroho ni ule ambao hakuna mtu mwingine anaweza kufanya kitu kwa ajili yako, Sio kumbukumbu ya uwezo ulinao bali ni uelewa wako wa juu , kufahamu imani ni nini, kuishi wakati uliopo. kusikia na kutenda kwa ajili ya kuishi nafsini mwako.
Uamusho wa kiroho unakuwepo tu kwenye uzoefu wako kupitia mwili wako, akili yako, na roho yako. sio kitu cha mara moja au tukio la mara moja. ni kitu cha kila siku. Ni kama maisha ya kawaida. ni kitu kisicho na mwisho.
Uamusho ni kujitambua , na kujiona kabisa kwamba unaishi kwa kupitia ufahamu wako, unakuwa makini wewe ni nani hasa, kipi ni kitu cha kweli. sio kitu cha changamoto. ni kitu cha maumivu makubwa. Ni kama moyo uliokuwa gizani na kwenda kwenye mwanga.
Lakini hizi hapa ni dalili za kweli za kujua kama wewe upo katika uamsho wa kiroho.
1.Nia yako ya kutafuta ukweli inakuwa juu

Macho yako yapo wazi na unaona mambo mengi yanafanyika. kwa hio utatamani kujua kila kitu. kwa kiasi, kwa umakini
2.Utakuwa makini na Chakula unachokula
Utakuwa makini kwa kila unachokula, iwe kula vizuri kwa ajili ya afya na mwili wako , kula kwa ajili ya roho yako ili uweze kukua unavyotaka. kula chakula cha akili yako ili kupata ufahamu zaidi.
3.Utakuwa Mwenye Huruma
Utaona huruma kwa watu, utaumia kwa ajili yao, utaona huruma hata kwa wanyama na viumbe wengine. unavaa viatu vyao unapoona jinsi wanavyohangaika.
4.Kitu fulani kitabadilika ndani yako.
Utaona badiliko la ufahamu wako, na kutokana na mtazamo huu mpya, kitu halisi kinaanza kubadilika ndani yako. Utafahamu ukweli halisi.
5.Utajisikia kubarikiwa.
unajisikia mwenye baraka ya ajabu hata kama hakuna kitu mbele ya macho yako. kile ulicho nacho hata kama ni kidogo kwako ni baraka kubwa. uwezo wa kujiona unaishi. uwezo wa kukaa mahali na kujifikiria , kufurahia uwepo ukiwa mwenyewe.
6.Kuwaelewa Watu na kutaka kuwasaidia pale.
Hutakuwa mtu wa kubishana , utakuwa ni msikilizaji mzuri, kwa kutambua kuwa sisi wote sio wakamilifu, hatujui kila kitu. utatamani kuwasaidia waamke mahali walipolala. utawafundisha kitu unachokijua.
7.Utakuwa mwenye Njaa ya kutaka kujua ukweli.
Utatembea katika ukweli, upendo wa kweli usio na sababu, mwaminifu, mtii ,uhalali. Utakuwa mbali na udanganyifu. Utakuwa mtu wa kujiuliza kwanini, kimetokea wapi, lini. utatamani kujua.
Dalili hizi ni tofauti kwa kila mtu. ni kitu cha upekee. wengine huona changamoto kubwa wanapokuwa wamefahamu ukweli na wanakuwa hawataki kuachilia udanganyifu.
Kuwapenda watu bila sababu , kuona kitu halisi, kuwa na hisia halisi ni kuwa na picha kubwa. Sio mtu wa kutazama nje yako au mtu mwingine kwa kuhukumu,kuwa mtu wa shukurani, amani na upendo.Kuwa makini kwa ajili yako, kuishi wakati ulipo.
Kama unajiona unauzoefu wa mambo hayo , wewe ni mtu wa uamusho wa kiroho.Sio mtu wa wasiwasi, woga na kujihisi kutojiunganisha na uwepo wa Mungu.
Kumbuka ,huu ni mwanzo tu , utaweza kuendelea kugundua mambo mengi kila wakati . Tafuta ukweli, tafuta upendo, kwenye hatua ya kujitambua wewe ni nani, Na ni kipi cha kweli.
Kwa Upendo Na Shukurani.
Mungu Akubariki.


No comments:
Post a Comment